+255 657036328
Lile sakata la Mzee yusuph, Amin salmin na Omary tego leo limeingia katika sura mpya baada ya mzee yusuph nae kujibu mambo kadhaa ambayo yalikuwa yakizungumzwa dhidi yake na wakurugenzi wenzie!.
MKURUGENZI WA JAHAZI MODERN TAARAB MZEE YUSUPH. |
Akizungumza na mtandao huu mfalme mzee yusuph alisema, kiukweli namshangaa sana Amin salmin amekuwa akisumbuka sana dhidi ya mimi mzee na bendi yangu ya Jahazi, nimemsoma kwenye mtandao wako akisema kuwa eti kamwe hawezi kuwa mfuasi wa mzee yusuph kwa kutengeneza nyimbo za dakika sita katika bendi yake ya T motto kama ambavyo mimi nimefanya katika nyimbo zangu mpya, kwanza aelewe kuwa hizo nyimbo sikumtungia yeye! nimetunga kwa ajili ya kuleta mabadiliko katika muziki wetu wa taarab na kubwa zaidi kuvuka mipaka ya nchi yetu na kufika mpaka afrika ya kusini.
MKURUGENZI WA T MOTTO MODERN TAARAB AMIN SALMIN. |
Yeye afanye awezavyo katika muziki asisumbuke na mimi!, kwani mimi namuumiza sana eeeh! maana haishi kunizungumzia kwenye mitandao kila kukicha!, mimi naijua thamani yangu kamwe huwezi kunifananisha na Amin salmin, mimi naujua muziki kwakuwa nimeusomea chuoni zanzibar, huyo Amin amesomea wapi muziki?, wala sisumbuki nae hanipi homa wala simuwazii, nafanya yangu tu!, thamani ya bendi yake ni sawa sawa na gari bovu linatafuta mvutaji...hana jipya!. Nasikia anataka kujibu hizo nyimbo zangu mbili, mimi nasema muache ajibu zaidi ya hizo ajibu tu, ila najua hana uwezo katika kutunga, aje mimi nimtungie shairi labda litamtoa, Nilipomuuliza ni shairi la aina gani atamtungia Amin salmin ili apeleke katika bendi yake ya T motto! alijibu ni mapema sana vuta subira!.
MKURUGENZI WA COAST MODERN TAARAB OMARY TEGO. |
sasa sasw mzee. kama wao mahodari sana wange unda hayo magari mabovu kwanza alafu wakaja kujibizana nae
JibuFuta