TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 11 Agosti 2015

EXELLENT MODERN TAARAB KUZINDUA BENDI PAMOJA NA ALBUM MBILI KWA MPIGO TAREHE 4/9/2015.

NA KAIS MUSSA KAIS.

             Bendi ya Exellent morden taarab yenye maskani yake mikocheni jijini dar, inatarajia kufanya uzinduzi wake siku ya tarehe 4/9/2015 katika ukumbi wa mikocheni resort "MRC" show itakayoanza saa mbili usiku hadi majogoo.


       Siku hiyo zitazinduliwa albam mbili kwa mpigo sambamba na kuizindua rasmi bendi hiyo ya taarab ambayo ni moto wa kuotea mbali kwa sasa hapa jijini dar!, Akizungumza na mtandao huu mkurugenzi wa bendi hiyo Mr Maimu alisema kuwa vijana wake wamejipanga kufanya mambo makubwa sana, ma-surprise bab-kubwa yameandaliwa kikubwa tunawaomba wadau na wapenzi wajitokeze kwa wingi kwani naamini watafurahi sana!.


    Katika uzinduzi huo bendi zitakazo sindikiza ni wakaliwao modern taradance, ogopa kopa classic bendi, omary tego na coast modern taarab, ruby bendi, pamoja na prince amigo tokea jahazi modern taarab, kiingilio kitakuwa ni shilingi elfu kumi tu mlangoni na utapata burudani zote hizo ndani ya jukwaa moja!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni