NA KAIS MUSSA KAIS.
Bendi yako uipendayo ya gusagusa min bendi wazee wa dollah!, siku ya leo jumapili wanatarajia kushusha burudani ya nguvu katika ukumbi wa hugo house kinondoni opposite na soko la ma-tx!.
Show hiyo ambayo imedhaminiwa na mamaa ya mujini, mamaa mtafutaji Asya Idarous khamsin chini ya kampuni yake ya fabak fashion inatarajia kuanza mapema sana tofauti na ilivyozoeleka!, akizungumza na mtandao huu bora Asya idarous khamsin alisema kuwa leo kuna surprise kibao zita-happen maeneo yale, masuper star wa mujini wengi watakuwepo sababu amewaalika kama kawaida. Anaomba wadau na wapenzi wa "Old is Gold" kujitokeza kwa wingi leo ili kumalizia week-end vyema!. Show hiyo ya leo mteja anatakiwa kutowa mlangoni kiingilio cha shilingi elfu tano tu na wala sio zaidi, ikumbukwe kuwa Asya khamsin ni mlezi wa bendi ya gusagusa na ni mshauri mkuu pia!, umeshapata bahati ya kumshuhudia Asya khamsin akiimba taarab asilia?, basi njoo leo umuone live!.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni