TANGAZA NASI

Breaking

Jumamosi, 8 Agosti 2015

KHADIJA KOPA AENDELEA KUNG'ARA...APEWA TUZO NA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

NA KAIS MUSSA KAIS.

             Malkia wa mipasho nchini tanzania khadija omary kopa, amepokea tuzo ya cheti cha utendaji kazi bora kwa shughuli za bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania na serikali kwa ujumla kwa kipindi cha mwaka 2010 mpaka 2015.


         Cheti hicho ambacho kimesainiwa na spika wa bunge alie maliza muda wake mama yetu Anna makinda ni kwa niaba ya bendi nzima ya ogopa kopa classic ambapo khadija omary kopa ni mkurugenzi wake!. Akitoa shukrani zake za dhati malkia huyo alisema anapenda kuishukuru serikali ya muheshimiwa Jakaya mrisho kikwete kwa kuthamini na kutambua mchango wake kwa jamii ya watanzania kupitia fani yake ya sanaa kwani wasanii tupo wengi sana lakini mpaka kupewa mimi hii kwangu ni heshima kubwa sana kwangu na kwa bendi yangu kiujumla alisema.


     Ikumbukwe kuwa pamoja na kushinda tuzo hii lakini malkia huyu ameingia katika shindano la "african muzik magazine award's" lililo na maskani yake nchini marekani na ameingia katika kipengere cha "best female east africa" hivyo wadau na mashabiki wa taarab tuendelee kumpigia kura kwa kuingia moja kwa moja katika mtandao wa www.afrimma.com/afrimma-nominees-2015/ hapo utaweza kumpigia kura na kumuwezesha kushinda.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni