TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 4 Agosti 2015

TETESI:- SALMA DOUBLE S, MAMAA WA TATU BILA AITOSA BAHARI MODERN TAARAB!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

                Muimbaji kiongozi wa bendi ya bahari modern taarab yenye maskani yake buguruni jijini dar Salma double S, a.k.a. mamaa wa tatu bila ameamua kuipa kisogo bendi ya bahari modern taarab na kuamua kukaa nyumbani huku akitafuta bendi ingine ya kujiunga nayo!.


         Muimbaji huyu mwenye sauti tamu anapokuwa anaimba, kwa sasa anatamba na wimbo wake maarufu uitwao "sura sio roho" uliotungwa nae hemedy omary ukipenda muite sonara wa maneno. sababu inayoelezwa kumfanya muimbaji huyu kuitosa bendi hii inayomilikiwa na mumewe wa ndoa Fikirini urembo ni kutothaminiwa na kudharauliwa pamoja na umuhimu mkubwa alionao muimbaji huyo ndani ya bendi hiyo.


    Mtandao huu uliamua kumtafuta kwa simu mmiliki wa bendi hii ambae ni mume wa Salma double S bwana fikirini urembo ili kujua kulikoni na je taarifa hizi zina ukweli wowote?, yeye alikuwa na haya yakueleza unajua ndugu mwandishi hizi taarifa ndio kwanza nazisikia kutoka kwako, salma bado yupo katika bendi na hakuna tofauti yoyote baina yetu labda umpigie simu salma mwenyewe akueleze, tulipomtafuta kwa simu Salma hakupatikana hewani, tunawaahidi wasomaji wetu kumtafuta salma ili adhibitishe taarifa hizi na tutawaletea hapa hapa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni