NA KAIS MUSSA KAIS.
Baada ya kufanya uzinduzi bab-kubwa wa albam ya sioni thamani ya pendo bendi yako ya wakaliwao modern taradance inatarajia kufanya onyesho la nguvu ikiwa sambamba na bendi ya twanga pepeta sugu ndani ya ukumbi wa kisasa zaidi wa Jm hall uliopo manzese tiptop jijini dar.
Akizungumza na mtandao huu mkurugenzi wa bendi ya wakaliwao modern taradance thabit abdul alisema kuwa vijana wake wamejiandaa vya kutosha kuwasambaratisha kabisa hao twanga pepeta, unajua hii ndio team masauti hatuna wasiwasi, kwa sasa tukutanishwe na bendi yoyote na tutawatoa nishai alijigamba thabit abdul.
Nae Luiza mbutu kiongozi na muimbaji wa bendi ya twanga pepeta alisema kuwa hatishwi na maneno ya thabit abdul kwani wao ni wakongwe katika sanaa ya muziki na wala hasumbuki na kelele za chura, ninachoongezea tu, nawaomba mashabiki wafike kwa wingi kwani tumepania kuwaonyesha kazi hawa watoto, siku hiyo tutapiga nyimbo zetu mpya kabisa pamoja na zile za zamani ambazo ziliwahi kupendwa.
Show hiyo ambayo inatarajia kufanyika siku ya ijumaa tarehe 14/8/2015 pale Jm hotel manzese tiptop kiingilio kitakuwa shilingi elfu nane 8000/= tu mlangoni na milango itakuwa wazi kuanzia saa mbili usiku wapenzi na mashabiki mnaombwa kufika kwa wingi ili mpate burudani ya nguvu kutoka katika bendi hizo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni