Bendi yako uipendayo ya gusagusa min bendi au ukipenda waite wazee wa UK!, wameamua kuhamisha show yao ya ijumaa ambayo ilikuwa ikifanyika pale max hall ilala jijini dar na kuipeleka hugo house kinondoni karibu na soko la ma-tx!.
BI AFUA SULEIMAN MUIMBAJI WA GUSAGUSA MIN BENDI. |
Akizungumza na mtandao huu mkurugenzi wa bendi hiyo Hassan farouk Hussein alifafanua kuwa wameamua kuhamishia show yao ya ijumaa pale hugo house sababu wadau, wapenzi na mashabiki wameomba kufanya hivyo kwa muda mrefu sasa nasi tukaona ni vyema tukawaridhisha, kwahiyo hugo kutakuwa na show mbili kwa wiki yaani ijumaa na ile show ya jumapili itaendelea kuwepo kama kawaida, na tunaanza ijumaa hii nakuendelea.
WAIMBAJI WA GUSAGUSA MIN BENDI. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni