TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 3 Agosti 2015

OMARY ZUNGU:- MAMA HAKUPENDA NIWE MWANAMUZIKI, NILIKUWA NAJIFUNZA KUPIGA KINANDA KWA KUJIFICHAFICHA SANA!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

                 Anaitwa omary zungu mpiga kinanda namba moja kwa sasa ndani ya ogopa kopa classic ambae amepiga kinanda nyimbo zote za albam ya mamaa mukubwa ambayo imekuwa gumzo kwa wadau na mashabiki kwa sasa kutokana na upigaji mzuri wa kinanda na sauti tamu toka kwa malkia khadija kopa.


OMARY ZUNGU AKIWA NA KINANDA.

     Mwandishi wa habari hizi alifanya mahojiano na msanii huyu ili kujua nini mafanikio yake katika muziki huu wa taarab mpaka sasa na je alianza vipi kupapasa kinanda?, ndugu mwandishi nilipata tabu sana kujifunza kinanda sababu wazazi wangu hawakupenda kabisa kuona mimi nakuwa mwanamuziki, nakumbuka mama yangu mzazi alinipigania sana nisiwe mwanamuziki, lakini ilishindikana sababu mimi muziki upo damuni sana.


        Nilikuwa natoroka nyumbani na kwenda katika bendi ya kaka yangu rajabu msekeni kujifunza upigaji wa kinanda wakati nayafanya hayo wazazi wangu walikuwa hawajui kabisa, nilihangaika hivyo hivyo kwa kujificha mpaka nilipoweza kupiga kinanda kwa ufasaha. kwa sasa nakula matunda ya uvumilivu wangu na nimekuwa nikiwasaidia wazazi wangu pia nashukuru mungu alisema!.


       Omary zungu pamoja na kupigia ogopa kopa classic bendi lakini pia ni muajiliwa wa bendi ya TOT inayomilikiwa na chama cha mapinduzi CCM, anasema katika wapigaji wa kinanda anamkubali sana thabit abdul na ndio mtu anaependa hata kumuiga upigaji wake.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni