TANGAZA NASI

Breaking

Jumamosi, 29 Agosti 2015

MAUA TEGO:-NILIMTOSA KAKA YANGU OMARY TEGO NA KUJIUNGA NA FIVE STAR'S KUFUATA MASLAHI ZAIDI.

NA KAIS MUSSA KAIS.

            Maua tego ni muimbaji maarufu sana katika muziki huu wa taarab nchini na alijipatia umaarufu zaidi kipindi yupo coast modern taarab alipotoa nyimbo za "Gubu la mawifi" na "kukupenda isiwe tabu", nyimbo zilizomtambulisha zaidi katika tasnia hii ya taarab nchini.


MAUA TEGO AKIWAPAGAWISHA MASHABIKI STEJINI.

       Nilipata nafasi ya kufanya mahojiano na muimbaji huyu pale mtoni mtongani jijini dar yalipo makazi ya bendi ya coast modern taarab, kwanza nilitaka kujua historia ya maisha yake katika muziki huu wa taarab, nae alikuwa na haya ya kuzungumza, nimeanza muziki huu wa taarab miaka 15 iliyopita katika bendi ya african music club bendi aliyokuwa akiimbia baba yangu mzazi pia na alienivutia zaidi ni baba yangu mzazi ambae ni marehemu kwa sasa.


      Baada ya marehemu baba yangu kuanzisha bendi ya coast modern taarab nikajiunga nae pia, alipofariki mzeebendi ikawa chini ya kaka angu omary tego ndipo nilitoka na wimbo wangu wa kwanza kabisa uitwao full kujiachia, lakini baadae nilihama na kujiunga na zanzibar star's modern taarab ambapo sikufanikiwa kurekodi kwa muda wote niliokuwepo pale. Nilirudi tena coast modern taarab nikafanikiwa kurekodi nyimbo zifuatazo:- kukupenda isiwe tabu, gubu la mawifi, damu nzito na mwanamke kujiamini ambazo zilinifanya niwe juu zaidi na bendi nyingi kuanza kuniwinda.


MAUA TEGO KATIKA UBORA WAKE.

     Ilipoanzishwa five star's ya mkurugenzi shark's nilijiunga nayo na kumuacha kaka yangu omary tego akibakia na coast modern taarab, lakini kikubwa kilicho nifanya niende five star's modern taarab ni maslahi zaidi nilitangaziwa kiasi kikubwa cha pesa nikaona ni vyema nikajiunga nayo, bahati mbaya bendi haikudumu nikarudi tena nyumbani coast modern taarab, na kwa sasa nina wimbo mpya kabisa unaitwa "mume ni bonge la issue" ambao upo jikoni unaandaliwa na ikiwa tayari basi wapenzi na mashabiki wangu watasikia kitu  roho inapenda.

OMARY TEGO NA MAUA TEGO.

     Ushauri wangu kwa wasanii tuache malingo, tuache kujisikia, mfano mzuri ni juzi juzi tu hapa baadhi ya wasanii tulichaguliwa kushiriki katika wimbo wa kuhamasisha wananchi kufanya kampeni kwa amani bila uchochezi na siku ya kupiga kula tujiepushe kukaa vikundi vikundi, lakini wale wasanii wanaojiona bab-kubwa hawakuja kushiriki kabisa! hili si jambo jema kabisa wasanii tuache malingo, tunaikosea jamii.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni