NA KAIS MUSSA KAIS.
Ule uzinduzi wa bendi pamoja na albam mbili kwa mpigo uliokuwa ufanyike siku ya tarehe 4 mwezi ujao na bendi ya exellent modern taarab umeahirishwa na kusogezwa tarehe za mbele zaidi.
Akizungumza na mtandao huu msanii mwandamizi wa bendi hiyo Maina thadei alithibitisha habari hii kwa njia ya simu baada ya kupigiwa ili azungumzie hili, ni kweli kaka uzinduzi umeahirishwa kwa sababu zilizo nje ya uwezo wetu, na siku chache zijazo tamko rasmi litatolewa kwa wadau na wapenzi wetu ili wajue ni wapi na ni lini tutafanya uzinduzi wetu. napenda kuchukuwa nafasi hii kuwaomba radhi wadau wa taarab na wapenzi wetu kwa mabadiliko haya yaliyojitokeza.
Mtandao huu unawaahidi kuendelea kufuatilia hili na kuwaletea tena taarifa na tarehe ya uzinduzi huo utakaofanyika baada ya kushindikana kwa huu wa kwanza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni