NA KAIS MUSSA KAIS.
Bendi ya zanzibar njema modern taarab kwa sasa ipo sokoni inauzwa kwa yeyote ambae atakuwa na fedha za kuinunua na kuliendeleza jina hilo basi anaweza kufanya hivyo!.
Tetesi hizi zimezagaa hapa jijini dar kwa sasa na mkurugenzi wa wakaliwao modern taradance thabit abdul alithibitisha hilo kwa kusema kuwa alipigiwa simu na mkurugenzi wa zanzibar njema modern taarab mr ally ngereja akimfahamisha kuwa bendi hiyo inauzwa, mtandao huu ulifanya jitihada kubwa za kumtafuta mr ngereja ili aweze kulithibitisha hili lakini kila alipopigiwa simu yake ilikuwa haipatikani juhudi zinaendelea kufanyika ili kumpata mkurugenzi huyo na kuuthibitishia umma wa wapenda taarab juu ya habari hizo.
Bendi ya zanzibar njema modern taarab, ndio ambayo alikuwa akiimbia marehemu ahmed mgeni na enzi ya uhai wake alitikisa sana na kibao chake "sitetereki" akiwa na bendi hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni