NA KAIS MUSSA KAIS.
Bendi ya wakaliwao modern taradance "team masauti au ukipenda unaweza kuiita timu ya taifa katika tasnia ya taarab kwa sasa hapa nchini inatarajia kufanya show ya nguvu ya utambulisho wa Hashim said tokea mashauzi classic sambamba na video mpya ya wimbo sioni thamani ya pendo siku ya jumamosi tarehe 19/9/2015 katika ukumbi wa mango garden kinondoni.
Akizungumza na mtandao huu mkurugenzi wa bendi hiyo thabit abdul mkombozi alisema kuwa katika onyesho hilo maalum watasindikizwa na bendi ya twanga pepeta sugu kisima cha burudani, excellent modern taarab, msagasumu na dogo jacky simela tokea jagwa music wataalam wa mnanda au mchiriku tanzania.aliendelea kusema kuwa nimeamua kufanya utambulisho wa hashim said pale mango garden sababu ni kiwanja ambacho hashim wamemzoea sanaa! na ana mashabiki lukuki.
Siku hiyo si yakukosa kwani kutakuwa na masuprise kibao toka kwa waandaji wa show hiyo ambao ni wakaliwao modern taradance wenyewe sambamba na blog bora ya taarab nchini tanzania ya ubuyuwataarabutz.blogspot.com.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni