TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 7 Septemba 2015

MOYO MODERN TARADANCE TOKA MKUBWA NA WANAWE, INGIZO JIPYA KATIKA TASNIA YA TAARAB NCHINI TANZANIA.

NA KAIS MUSSA KAIS.

            Moyo modern taradance ni ingizo jipya kabisa katika tasnia hii ya taarab nchini, bendi iliyo chini ya kituo cha mkubwa na wanawe kinachoongozwa na mkubwa fellah! akishirikiana na meneja chambuso.



WAIMBAJI WA MOYO MODERN TARADANCE KATIKA POZI LA PAMOJA.

         Kuanzishwa kwa bendi hii kumeleta ushindani mkubwa sana kwa bendi zilizopo hususani kiburudani na kibiashara zaidi, Director wa bendi hii ni mgeni kisoda mwanamuziki ambae hapo kabla alikuwa katika bendi ya jahazi modern taarab.moyo modern taradance imekuwa ikijifua kwa kutengeneza nyimbo zao mpya kabisa miongoni mwa nyimbo hizo ni Dongo la gizani mwimbaji mwajuma kidoti na ya pili ni Twaomba salama muimbaji ni mbogo waukweli.wakati huo huo muimbaji Thania msomali na Amina mnyalu nao ni miongoni mwa waimbaji wapya wa bendi hiyo.

WANAITWA MOYO MODERN TARADANCE-WATOTO WA SAID FELLAH.

        Bendi hii inatarajia kufanya onyesho lake la kwanza siku ya tarehe kumi na moja mwezi huu wa tisa katika ukumbi wa dar live mbagala katika kuwasindikiza kaka zao wa yamoto bendi wakati wa uzinduzi wa video ya wimbo wao mpya. karibuni sana moyo modern taradance.


       

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni