Siku ya jumamosi team nzima ya Jahazi morden taarab walikua wakitoa burudani kwa mashabiki zao wa Moshi.
Kwa
mujibu wa Mzee Yusuph anasema kuna mtu alikuja akawa anataka kuingia
bure na kujitapa kwamba yeye halipi.Baunsa akaanza kujibishana nae na
kumueleza kwamba haiwezekani kuingia bure.
Baada ya kuambiwa hivyo huyo mtu aliweza kuondoka kisha akarudi tena
kwa mara ya pili akalipa hela ya kiingilio akaruhusiwa kuingia. Lakini
baada yakuingia hakukaa sana ndani akarudi tena kwa baunsa na kuanza
kumtolea lugha ya matusi,awali baunsa hakuweza kumjibu kitu ila mwishowe
baunsa alimwambia “wewe tukana najua leo umekuja na gari ya shemeji”
maneno ambayo yalimkera huyo jamaa na kuamua kumpiga baunsa ngumi ya
shingoni hapo ndipo ugomvi ulipoanzia na mwishowe jamaa akatoa bastola
nakumpiga baunsa risasi.
Kwa sasa mtu huyo anashikiliwa na polisi na baunsa yupo katika hospitali ya KCMC akiendelea na matibabu...Habari kwa hisani ya Geah habib wa cloud's fm.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni