NA KAIS MUSSA KAIS.
Thania msomali ni mwanamuziki muimbaji anae chipukia na kwa sasa ndio jicho la bendi mpya ya "moyo modern taradance" inayoongozwa na mkubwa fellah chini ya director mzoefu mgeni kisoda ambae hapo kabla alikuwa ni msanii wa jahazi modern taarab.
|
THANIA MSOMALI. |
Nilipata bahati ya kufanya mahojiano na muimbaji huyu pale katika kambi yao ya moyo modern taradance maeneo ya temeke, kwanza alianza kwa kuelezea historia yake kimaisha. Nimezaliwa miaka 30 iliyopita mkoani tanga, nimesoma katika shule ya msingi muguga iliyopo kikuyu nairobi nchini kenya, baada ya hapo nikasoma secondary katika shule ya eckenford nikamaliza mwaka 2005, wazazi wangu wakanipeleka chuo cha saint joseph nikasomea fani ya usekretari.
Maisha yangu ya muziki chanzo haswa ni kuvutiwa na uimbaji wa bi rukia ramadhan na sabaha salum muchacho, akina mama hawa nilikuwa nawapenda sana na ndio sababu ya mimi pia kuimba muziki huu wa taarab ingawa wazazi wangu hawapendi kuona mimi nikiimba, bendi yangu ya kwanza kuifanyia kazi ni five star's modern taarab ambayo nilijiunga nayo mwaka 2010.
Baadae nilihama na kujiunga na bendi ya T motto mwaka 2012 iliyokuwa ikiongozwa na meneja kais mussa kais wakati huo hapo nilikutana na akina jokha kasim, marehemu nyawana fundikira na aisha masanja, hapo nilikaa takribani miaka miwili baadae niliondoka na kujiunga na bendi ya mashauzi modern taradance safari yangu yote hiyo sikuwahi kubahatika kurekodi wimbo wowote ingawa nilikuwa naimba vizuri.
Niliamua kuachana na mashauzi classic na kuwa msanii huru ndipo niliporekodi wimbo wangu wa kwanza kama msanii huru wimbo uitwao "hivi ndivyo nilivyo" ambao unaendelea kufanya vizuri katika media mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi.kwa sasa nipo katika bendi yangu mpya moyo modern taradance na tayari tuna nyimbo 4 mpya kabisa.tunawaomba wapenzi wetu watupe sapoti kwani tumepania kuleta mabadiliko katika muziki wetu huu wa taarab nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni