TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 18 Septemba 2015

HASHIM SAID ACHAGULIWA KUWA DIRECTOR WA WAKALIWAO MODERN TARADANCE!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

                Hashim said Igwee, ambae kwa sasa wapenzi kadhaa wa mashauzi wamempachika jina la "yuda eskarioti" baada ya kuihama bendi hiyo na kujiunga na mahasimu wao bendi ya wakaliwao modern taradance, amechaguliwa kuwa director na bendi master wa wakaliwao.


HASHIM SAID NA THABIT ABDUL.

           Akizungumza katika kikao cha bendi hiyo mkurugenzi wa wakaliwao modern taradance thabit abdul alimteua hashim said kuwa director mpya wa bendi ya wakaliwao kutokana na uzoefu mkubwa alionao hashim katika tasnia hii, unajua mtu kama hashim unapompa uongozi ndani ya bendi unakuwa na amani kubwa kulingana na utendaji wake alisema thabit abdul.


      Nae hashim akiushukuru uongozi wa wakaliwao alisema kuwa nitaifanya kazi hii kwa bidii kubwa na kuhakikisha kuwa wasanii wa wakaliwao wanakuwa na nidhamu ndani na nje ya steji, mimi hii si mara ya kwanza kuwa na cheo hiki hata kule nchi jirani pia nilikuwa na cheo kama hiki kwahiyo najua nini nakifanya ninapokuwa madarakani alisema hashim said Igwee.


         Wakati huo huo siku ya kesho jumamosi ndani ya mango garden wakaliwao modern taradance wakishirikiana na twanga pepeta, excellent modern taarab, msagasumu na dogo jack simela watafanya onyesho la nguvu katika kumtambulisha rasmi hashim said ndani ya bendi hiyo pia kutambulisha rasmi video ya albam ya sioni thamani ya pendo kwanzi na mashabiki wanaombwa kujitokeza kwa wingi sana kupata burudani hiyo, kiingilio ni shilingi 10,000 tu!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni