TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 28 Agosti 2015

ASYA MJUSI:- NILISIMAMISHWA KAZI EAST AFRICAN MELODY KWA SHINIKIZO LA MDAU!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

              Asya mjusi ni muimbaji nyota anaechipukia kwa kasi ya ajabu kwa sasa akiwa na bendi ya wakaliwao modern taradance, Asya mjusi amekuwa na safari ndefu kiasi katika tasnia hii ya taarab nchini tanzania.


ASYA MJUSI.

        Muimbaji huyu alianza muziki mwaka 2008 enzi hizo akiwa na bendi ya king's modern taarab yenye maskani yake mburahati jijini dar, ilipofika mwaka 2010 nilijiunga na bendi ya victoria modern taarab tukiwa na akina mwanahawa chipolopolo na mwanne othman ambae kwa sasa ni mtangazaji wa east africa redio. Pale sikukaa sana kwani ilipofika mwaka 2011 mwishoni nilijiunga na bendi ya east african melody.


      East african melody nilipatwa na jambo ambalo naweza kusema kuwa ni udhaifu wa baadhi ya viongozi kama sio kiongozi katika maamuzi, kuna mdau mmoja ambae nisingependa kumtaja jina alikuwa akijishuku kuwa mimi kila ninapokuwa naimba stejini basi eti namrusha roho yeye kitu ambacho si cha kweli kabisa, nyimbo za melody mimi nimezikuta na hata zingine aliekuwa ametunga simjui leo hii iweje aseme kuwa nikiimba namrusha roho yeye!, jambo lingine program ya nyimbo stejini sipangi mimi zinapangwa na director, sasa naanzaje kumrusha roho?.

ASYA MJUSI.

      Ilifikia wakati yule mdau ambae ni mwanamke alienda hadi kwa uongozi wa melody akashitaki, uamuzi uliochukuliwa ni mimi kusimamishwa kazi eti sababu namrusha roho mdau haya ni maajabu kabisa!, unaanzaje kunisimamisha kwa tatizo lisilonihusu?. nashukuru mungu kwani siku zote likuepukalo lina heri kwako!, kwa sasa nipo zangu wakaliwao modern taradance na nina wimbo mpya unaitwa "KUSUDI HAINA POLE" ambao nitaurekodi hivi karibuni. huo wimbo ukishatoka nao aseme kuwa namrusha roho yeye...mimi sijari nipo kikazi zaidi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni