TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 26 Agosti 2015

WASANII WA MASHAUZI CLASSIC WAVAMIA JUKWAA LA WAKALIWAO MODERN TARADANCE KABAKABANA!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

              Katika kile kinachoonekana ujirani mwema na upendo uliotukuka toka kwa wasanii, siku ya jumanne tarehe 25/8/2015 katika ukumbi wa kabakabana baadhi ya wasanii wa bendi ya mashauzi classic walivamia jukwaa la wakaliwao modern taradance na kupiga wimbo wa bonge la bwana ulioimbwa nae Hashim said "Igwee" ambae nae alikuwa mashauzi hapo kabla.


J4 BOYA NA KALI KITIMOTO WA MASHAUZI CLASSIC WAKIWA STEJI YA WAKALIWAO.

       Ilikuwa ni muda wa saa saba na robo usiku baada ya Hashim kuimba wimbo mmoja walionekana wapiga vyombo wa mashauzi J4 boya na kali kitimoto wakipanda stejini na kumuomba Hashim said asishuke stejini na ndipo walipompigia wimbo wa bonge la bwana na Hashim kuanza kuimba kwa furaha kubwa sana. tukio hili liliwafanya wapenzi na mashabiki kulipuka kwa mayowe na vifijo sababu bendi hizi kwa siku za karibuni zimekuwa mahasimu wakubwa mpaka kufikia wakurugenzi wakuu kutosalimiana.

KALI KITIMOTO AKIWAJIBIKA KATIKA STEJI YA WAKALIWAO.

     Alisikika mshabiki mmoja akisema kuwa namna hii ndio inapendeza sio uhasama usio na msingi kila kukicha mitandaoni tumechoka!, unajua viongozi wa mabendi ndio wanafanya tasnia hii kuwa ngumu, msanii akija kuwasaidia wakaliwao tokea mashauzi basi siku ya pili utasikia kasimamishwa! au msanii akitoka wakaliwao kwenda kuwasaidia mashauzi nae siku inayofuata anasimamishwa kazi! huu si uungwana na wala sio maadili katika sanaa!, nawapa big up mashauzi kwa hiki walichofanya leo!.


J4 BOYA WA MASHAUZI AKIFANYA YAKE KATIKA STEJI YA WAKALIWAO.

       Ukiondoa kali kitimoto aliepiga kinanda na J4 boya aliepiga gita la besi vile vile walikuwepo wacheza viduku wanne tokea mashauzi classic ambao nao walicheza wimbo huo wa bonge la bwana wakati Hashim saidi akiimba stejini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni