TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 23 Agosti 2015

WAKALIWAO MODERN TARADANCE "TEAM MASAUTI" KUANZA MAZOEZI YA NYIMBO MPYA KESHO JUMATATU.

NA KAIS MUSSA KAIS.

            Bendi yako uipendayo ya wakaliwao modern taradance au "team masauti" siku ya kesho jumatatu inatarajia kuanza mazoezi ya nyimbo mpya kwa wasanii wapya ambao wamejiunga na bendi hiyo hivi karibuni.


         Akizungumza na mtandao huu makini mkurugenzi wa bendi hiyo thabit abdul "mkombozi" alisema kuwa mazoezi hayo ni maalum kwa vigongo vipya kabisa kwa wasanii wapya ndani ya bendi yangu, kila mmoja nitamtengenezea wimbo mzuri kama kawaida yangu na ndio maana nikaitwa mkombozi. mazoezi hayo ambayo yatafanyika katika ukumbi wa kabakabana mwananyamala A jijini dar yatajumuisha wasanii wapya ambao ni kibibi yahya toka maja's modern taarab, salha wa hammer tokea five star's, asya mjusi tokea east africa melody, hashim said tokea mashauzi classic, hafidh faith tokea east africa melody, aisha vuvuzela tokea maja's modern taarab pamoja na wale wasanii wa zamani.


      Alizitaja nyimbo hizo mpya na waimbaji wake kuwa ni:-


                                  1.Ukinuna uwe na sababu- Aisha othman vuvuzela.

                                  2.Kwangu old fashion- Kibibi yahya

                                  3.Najuta kukufahamu- Hashim said

                                  4.Mbaya halisi na wema hakosi- Salha wa hammer Q

                                  5.Kusudi haina pole- Asya mjusi

THABIT ABDUL AKIWA MSANII MPYA WA BENDI HIYO HASHIM SAID IGWEE!.
   

       Nyimbo zote hizo zimetungwa nae thabit abdul mkombozi mkurugenzi wa bendi hii ya wakaliwao modern taradance, wadau, mashabiki na wapenzi tusubiri kwa hamu kuona ujio huu mpya wa team masauti kwani kwa sasa ndio bendi iliyo midomoni mwa wapenda taarab afrika mashariki na kati.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni