TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 20 Agosti 2015

HATIMAE YAMETIMIA:- NDOA YA HASHIM SAID "IGWEE" NA FATU CHINA YAVUNJIKA RASMI.

NA KAIS MUSSA KAIS.

           Ndoa ya aliekuwa muimbaji wa mashauzi classic hashim said na fatu china hatimae imevunjika rasmi  baada ya kutofautiana na kuwa mbalimbali kwa muda wa miezi minne.


HASHIM SAID NA FATU CHINA ENZI ZA MAPENZI YAO.

      Habari za uhakika zilizotufikia katika mtandao wetu zinasema kuwa ndoa hiyo ilianza misukosuko miezi kadhaa iliyopita jambo lililopelekea wanandoa hao kutokuwa na maelewano mazuri, Dawati letu la habari baada ya kupata habari hizi lilimtafuta Hashim saidi na kumuuliza ukweli halisi wa jambo hili uko vipi?.


MAMA MARIAM MZAZI MWENZA WA HASHIM SAID AMBAE NI MKEWE KWA SASA.

     Ni kweli kwa sasa mimi na fatu china hatuna uhusiano wowote nikimaanisha si mke wangu tena, yeye ana maisha yake na mimi kwa sasa nina maisha yangu, baada ya kutengana rasmi na fatuma niliamua kumrejea mzazi mwenzangu na tayari ndoa imefungwa tena baina yangu na yeye na nafurahia sana maisha haya sababu nipo karibu na watoto wangu na mzazi mwenzangu pia.

FATU CHINA ALIEKUWA MKE WA HASHIM SAID AKIWA KATIKA UBORA WAKE.

    Yaliyotokea nyuma kati yangu na fatu china nayaona ni kama changamoto tu katika maisha na namtakia maisha mema huko alipo sina tatizo nae kabisa alimalizia kwa kusema. mtandao huu ulimtafuta fatu china kwa njia ya simu ili nae azungumzie hili lakini hakupatikana muda wote simu ilikuwa imezimwa tunaendelea kufanya jitihada ili kuweza kumpata fatuma nae azungumzie jambo hili.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni