TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 19 Agosti 2015

HASHIM SAID AACHA KAZI RASMI MASHAUZI CLASSIC NA YUPO KATIKA MAZUNGUMZO NA BENDI YA......!.

NA KAIS MUUSA KAIS.

               Muimbaji wa kutegemewa wa bendi ya mashauzi classic ambayo inaongozwa na Isha mashauzi au jike la simba kama anavyofahamika na wapenzi wake, Hashim said au Igwee! ameamua kuachana na bendi yake hiyo na taarifa za chini ya kapeti ambazo ni za uhakika inasemekana kwa sasa yupo katika mazungumzo na bendi moja maarufu sana hapa dar wakifanya makubaliano ya mwisho ili ajiunge nayo.


HASHIM SAID IGWEE!.

       Kisa cha Hashim said kuamua kuachana na bendi ya mashauzi classic haikujulikana sababu hata mwenyewe anasema kuwa hana tatizo na kiongozi wala msanii yeyote katika bendi hiyo ila ameamua yeye mwenyewe kwa ridhaa yake kuachana na bendi hiyo kwani miaka minne aliyoitumikia inatosha sana kwake.


HASHIM SAID AKIWA STEJI.

     Akizungumza na mtandao huu kwa njia ya simu Hashim saidi alisema sikupata shindikizo la aina yoyote toka kwa yeyote ila ni maamuzi yangu tu na naomba yaheshimiwe, mimi ni mtu mzima na sifundishwi jambo wala maamuzi hiyo ndio hali halisi, ikumbukwe kuwa jana mchana Hashim said alituma sms kwa baadhi ya watangazaji wa taarab nchini akiwajulisha kuwa hayupo tena mashauzi classic na pia alituma sms hiyo katika mtandao huu kuwajuza wasomaji wake.Tulipompigia simu Hashim kutaka kujua ni wapi anaelekea maana kuna taarifa kuwa yupo katika mazungumzo na moja ya bendi maarufu hapa jijini, alisema kwa sasa napumzika ila naweza kuwa na maamuzi hapo baadae.



       Mtandao huu unawaahidi wasomaji wake kuendelea kuwaletea mlolongo mzima wa tukio hili zito toka kwa Hashim said ili mjue baada ya kuiacha mashauzi ni wapi anaelekea? tuendelee kuwa pamoja.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni