TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 24 Septemba 2015

BENDI MPYA WAKALI WA TOWN MODERN TAARAB WAINGIA KAMBINI RASMI BAGAMOYO.

NA KAIS MUSSA KAIS.

            Bendi mpya nchini tanzania wakali wa town modern taarab imeingia kambini rasmi leo katika hotel ya kifahari pembezoni mwa bahari ya hindi huko bagamoyo mkoani pwani tayari kwa maandalizi ya albam yao mpya iitwayo "heri ya mchawi kuliko ndugu shetani".


FADHILA MNOGA MUIMBAJI MPYA WA WAKALI WA TOWN.

         Akizungumza na mtandao huu makini mkurugenzi wa bendi hiyo Mr vam au ukipenda muite "tajiri mtoto" alisema kuwa ameamua kuweka kambi bagamoyo sababu ni sehemu iliyotulia na isiyo na bughuza za aina yeyote ile, bendi yangu ina waimbaji wachanga ila wana vipaji vya hari ya juu sana, sitaki kuwatumia hawa waimbaji wenye majina makubwa sababu ni wasumbufu sana. albam yetu mpya itakuwa na nyimbo sita na itaitwa "heri ya mchawi kuliko ndugu shetani". 


        Aliendelea kwa kusema muimbaji fadhira mnoga nimemchukua kutoka katika bendi ya G5 modern taarab na ataimba wimbo huo utakaobeba albam, nakaribisha waimbaji wapya na wenye vipaji nitawasaidia wanipigie simu yangu namba 0712-311350.alimalizia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni