NA KAIS MUSSA KAIS.
Bendi yako uipendayo wakaliwao modern taradance "team masauti" imetoa ratiba yao katika kusherehekea sikukuu ya idd-el-hajj ni kiwanja kipi na kipi watakuwa wakitumbuiza.
Akizungumza na mtandao huu makini mkurugenzi wa bendi hiyo thabit abdul "mkombozi" alisema kuwa siku ya idd mosi tarehe 24/9/2015 watakuwa katika ukumbi wa nikkita resort mbezi beach maeneo ya jogoo, siku ya idd pili tarehe 25/9/2015 watakuwa katika ukumbi wa kabakabana mwananyamala A, na siku ya idd tatu tarehe 26/9/2015 watakuwa katika ukumbi wa center grill zamani flamingo pale maeneo ya magomeni mwembe chai, wapenzi na wadau wetu tujumuike kwa pamoja alimalizia kwa kusema.
Wakaliwao modern taradance kwa sasa wana vibao vipya kabisa ambavyo bado havijarekodiwa ila wamekuwa wakipiga katika kumbi mbalimbali wanapofanya maonyesho yao, wapenzi mnaombwa kufika kwa wingi katika maonyesho hayo yote na kiingilio cha mlangoni kitakuwa ni shilingi elfu tano tu 5000/= za kitanzania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni