NA KAIS MUSSA KAIS.
Bendi mbili za fungakazi modern taarab na rocky city modern taarab wakurugenzi wake wamefikia makubaliano ya kuungana kwa pamoja katika shughuli zao za burudani kwenye kumbi mbalimbali.
|
FUNGAKAZI MODERN TAARAB. |
Wakizungumza na mwandishi wa habari hii wakurugenzi hao kapten temba na kanal muhsin kwa pamoja wamesema kuwa wamefikia makubaliano hayo ya kuwapa burudani wadau na wapenzi wao kwa pamoja ili kujenga umoja na upendo baina yao, unajua hapo kabla tuliwahi kuwa pamoja katika bendi ya fungakazi modern taarab kanal muhsin akiwa kama meneja ila baadae akaniomba kuanzisha bendi yake ya rock city nami nilimruhusu, na sasa tunaungana tena, kwakweli inapendeza sana alisema kapten temba.
Nae kanal muhsin kwa upande wake alisema kuwa natambua sana uwezo wa kapten temba katika utunzi na namuheshimu sana hivyo kwa kuungana tena na yeye, mimi binafsi yangu na wasanii wa rocky city kwa ujumla tumefurahishwa sana. wakifafanua muungano wao walisema kuwa kwa show za kuandaa wenyewe watakuwa pamoja na kushirikiana ila zile show za kununuliwa basi kila bendi itakwenda kivyake labda kama promota akiamua kuwachukuwa kwa pamoja basi watakuwa wote.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni