TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 7 Oktoba 2015

KAIS MUSSA KAIS:- MDAU ANAETAKA KUSAFIRI NA WAKALIWAO NAIROBI KENYA, AWASILIANE NAMI KWA MAELEZO ZAIDI.

NA MWANDISHI WETU.

                 Safari ya wakaliwao modern taradance kuelekea katika tamasha la kimataifa la coast night nchini kenya inatarajia kuanza alhamisi ya tarehe 5/11/2015 na siku ya pili yaani tarehe 6 ijumaa ndio siku ya show husika.


KAIS MUSSA KAIS MENEJA MIPANGO NA URATIBU WA WAKALIWAO.

         Meneja mipango na mratibu wa bendi hiyo kais mussa kais ameuambia mtandao huu  kuwa uongozi umetoa nafasi za upendeleo kwa wadau na mashabiki wa bendi hiyo kusafiri na kwenda kujionea mambo makubwa ambayo bendi hiyo imepanga kuyafanya katika tamasha hilo, utaratibu kwa wapenzi wa bendi hiyo kusafiri ni kwa kuchangia gharama kidogo kama ifuatavyo, kwa mtu mmoja anatakiwa kuchangia shilingi laki moja na ishirini ambayo ni nauli, na mchanganuo wa pesa hizo ni kama ifuatavyo. 70,000/= nauli ya kwenda na kurudi, 20,000/= pesa ya hotel kwa siku moja, 10,000/= ni pesa ya kuingia katika tamasha, 20,000/= ni pesa ya kutafutia paspot ya muda kwa ajili ya kuruhusiwa kuingia nchini kenya.


            Hii ni nafasi pekee na itakuwa kwa mara ya kwanza bendi kutoka tanzania kuingia na wadau na mashabiki wake katika tamasha hilo kubwa na la kipekee afrika mashariki na kati, yeyote atakaekuwa tayari kujiunga na wakaliwao kuelekea kenya basi awasiliane nami kais mussa kais kwa namba yangu ya simu 0657-036328 mapema zaidi ili niweze kufanya mchakato wa usafiri mapema kwani gari ya wasanii itakuwa tofauti na gari ya wapenzi na wadau watakaokuwa tayari kwenda alimalizia kwa kusema. 


               

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni