TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 7 Oktoba 2015

TETESI:- OMARY ZUNGU WA OGOPA KOPA NA AMINA MNYALU WA MOYO BENDI...MAPENZI MOTOMOTO?.

NA KAIS MUSSA KAIS.

                     Omary zungu ni mpiga kinanda namba moja wa bendi ya ogopa kopa ya jijini dar pia ni muajiliwa wa bendi ya T.O.T, siku za hivi karibuni ameonekana maeneo nyeti akiwa na muimbaji wa bendi mpya ya moyo modern taarab inayoongozwa na director mgeni kisoda.


OMARY ZUNGU MPIGA KINANDA WA OGOPA KOPA CLASSIC.

            Mtandao huu uliunda kamati ya udaku ambayo ilianza kufuatilia nyendo za wawili hawa bila wenyewe kujijua na kuweza kuwabamba mara kadha pale Jm hotel manzese na Center grill zamani flamingo wakiwa katika mahaba mazito, mwandishi wetu alipotaka kuwapiga picha walijinasua na kujifanya kama ni watu ambao walikuwa wakitia stori za kawaida!.


        Hatukuishia hapo mwandishi wetu alipanga safari mpaka buguruni anapoishi omary zungu na kuanza kuwadadishi baadhi ya majirani ambao wanaishi nyumba moja na mpiga kinanda huyo na kufanya mahojiano nae je amekuwa akimuona Amina mnyalu akiingia chumbani kwa omary ama lah? na je kwanza anamfahamu huyo Amina mnyalu? akijibu kwa sharti la kutoandikwa jina lake mpangaji huyo alisema kuwa namjua vyema amina mnyalu kwanza alikuwa bendi ya king's modern taarab baadae alienda maja's modern taarab kabla ya kuhamia bendi ya fellah aliyopo sasa, kiukweli mimi huwa namuona sana hapa kwa omary na kiukweli watakuwa ni wapenzi sababu huwa hadi zamu za kufagia huwa tunabadilishana nae mara kibao tu!.

AMINA MNYALU MUIMBAJI WA MOYO MODERN TAARAB.

          Ila wakati mwingine huwa anakuja analala na kuondoka asubuhi na wakati mwingine huwa tunashinda nae hapa nyumbani akiwa na omary, tafadhali nakuomba usinitaje mwenzangu sitaki kusutwa mie na ukubwa huu akaah!.mtandao huu baada ya kupata taarifa hizi zenye uhakika kwa asilimia themanini tuliwatafuta wapenzi hawa kupitia simu zao za mkononi kuthibitisha haya lakini hawakupatikana hewani, tunawaahidi wasomaji wetu kuwaletea sehemu ya pili ya sakata hili, je ni kweli Omary zungu na Amina mnyalu ni wapenzi?...Tuvute subira!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni