TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 9 Oktoba 2015

OMARY ZUNGU AVAMIA OFISI ZA UBUYU WA TAARAB NA KUKANA KUWA NA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA AMINA MNYALU!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

                   Kufuatia habari ambayo iliandikwa siku ya jumatano tarehe 7/10/2015 na mtandao huu, yenye kichwa cha habari "omary zungu wa ogopa kopa na amina mnyalu wa moyo bendi penzi motomoto?" leo majira ya saa saba mchana omary zungu alivamia ofisi zetu huku akiwa na hasira kali na kukanusha habari zile kwa kutoa ufafanuzi ufuatao:-


OMARY ZUNGU.

         Mimi sina mahusiano yoyote ya kimapenzi na huyo amina mnyalu ukweli halisi ndio huo, ukaribu uliopo baina yangu na amina ni wa kikazi tu na wala si vinginevyo. Amina ana wimbo wake ambao anataka aimbe nje ya bendi yake, sasa amenichagua mimi ndio nimpigie kinanda kwahiyo mara nyingi tumekuwa tukikutana na kupeana sauti za uimbaji na wakati mwingine hata kurekebisha baadhi ya mistari ya mashairi yake!, ile habari imeniharibia mambo mengi sana kiukweli naomba muwaeleze  wananchi kuwa sikweli tafadhali.


         Ndipo tulipoamua kumpigia amina mnyalu simu yake ya mkononi ili nae azungumzie hili lakini alikuwa na majibu ya mkato na maneno ya kashfa na matusi ambayo hayafai kuyaandika humu kimaadili ya kazi yetu ya uandishi wa habari, ila kifupi nae alikuwa anakataa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na omary zungu zaidi ya project ambayo wanatarajia kuifanya hapo baadae!, ubuyu wa taarab unawaomba radhi kwa usumbufu wowote ambao wameupata kwa namna yoyote ile!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni