TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 13 Oktoba 2015

WAMILIKI NA VIONGOZI WA TAARAB NCHINI, WAYALALAMIKIA MAKAMPUNI KWA KUTOWATHAMINI NA KUWAJALI.

NA KAIS MUSSA KAIS.

                   Wamiliki na viongozi wa bendi za taarab nchini tanzania wametoa malalamiko yao kwa makampuni mbalimbali yanayodhamini vipindi vya taarab katika redio na televisheni mbalimbali nchini kuwa hazitendi haki kwa kuzinyanyapaa bendi za taarab katika suala zima la udhamini.


           Wakizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wa habari hizi wamiliki na viongozi hao walisema kuwa wamekuwa wakishangazwa sana na khali hii na kujiona kama ni watu wanaotengwa na makampuni hayo!, akitolea mfano kiongozi mmoja ambae ni meneja kwenye moja ya bendi kubwa sana ya taarab hapa nchini alisema kuwa, aliwahi kupeleka "propozo" ya kutaka wadhaminiwe katika tour yao ya mikoa sita ya hapa nchini na humo kote watakapokuwa wakipita watakuwa wakitangaza kinywaji husika kama wadhamini wa safari hiyo lakini cha ajabu tokea mwaka jana mpaka sasa hakuna majibu yoyote, ila katika redio wamekuwa wakidhamini kwa pesa nyingi sana hii si haki, wakumbuke kuwa sisi ndio tunaozalisha hizo nyimbo ambazo wao wanaziona zinafanya vizuri mpaka kufikia kuwapa redio mamilioni ya pesa.


            Mmiliki mmoja mwenye itikadi kali alisema wapo njiani kuunda chama chao ili kiweze kuwatetea katika kudai haki zao kisheria ikiwemo redio kuwalipa kila wanapocheza nyimbo zao redioni, labda kwa njia hii wataweza kugawana huo udhamini wanaoupata wao redio na televisheni kupitia makampuni haya alimaliza kwa uchungu. Makampuni tofauti yamekuwa yakitoa sapoti kubwa sana kwa media mbalimbali nchini kwa kudhamini vipindi vya taarab ambavyo vimekuwa vikirushwa kila siku.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni