NA KAIS MUSSA KAIS.
KWA wapenzi wanaoufatilia kwa undani mziki wa
asili wa mnanda hapana shaka kushindwa kumfahamu nguli wa mashairi ya
mnanda,Hamza Hamisi 'Gobole'.
Maadhi
yake yote ya mziki wa mnanda ni asili ukianzia kwenye ala za mziki mwenye. Kama
unavyojuwa mnanda hutumia ngoma,visoda,malimba na vitu vingine vya asili,ili
kunogesha mziki huu.
Mnanda
ndio mziki wetu wa asili ya kitanzania na ndo maana marehemu Omari Omari
alikubalika Africa kusini alipoenda kufanya shoo Johannesburg kwa kuimba nyimbo
za asili yetu,ambayo ni mnanda.
|
MR GOBOLE!. |
Enzi za uhai wake mfalme huyu wa mnanda
marehemu Juma Juma 'Lupozi' aliwahi kusema kuwa anakipaji çha kuzaliwa nacho.Marehemu
lupozi alimuamini gobole katika utungaji wa nyimbo zake baada ya kuona kazi
alizofanya na omari omari.
Gobole alizaliwa 1976
jijini Dar es salaam na kupata elimu yake ya msingi kwenye shule ya msingi
Dundani iliyopo mkuranga,na kujiunga na sekondari mînaki kisawe mkoani pwani.
Unaweza ukasema
maisha ya Gobole ni ya kisanaa toka akiwa shule ya msingi alipokuwa anatunga
mashairi ya darasa na shule.
Kwa muda wote yupo
shule alikuwa akipendelea kupeleka mashairi kwenye magazeti na redio. Alikuwa
anapeleka magezeti ya nipashe na alikuwa anafanîkiwa kupewa nyota kwenye
mashairi yake.
Wakati huo ukipeleka
shairi kwenye magezeti ili upate ela lazima uwe na nyota kwenye shairi lako.na
tukipewe 4000 kwa shairi.
Hakika kwa muda
huo,ilikuwa ngumu kupata nyota kulinga na wimbi la watunzi wa mashairi wenye
uwezo walikuwa lukuki. Mbali na kupeleka tungo zake magazetini,pia alikuwa
anapeleka redio Tumaini kwenye kipindi cha 'Chimbua chimbua' ingawa huku
mashairi yake mengi nayo yalipata kusomwa.
Baada ya watu
kuzitambua kazi zake kwa undani,ndipo mwaka 2000,marehemu Omari Omari akakutana
nae kwenye mchakato wa kutunga nyimbo za kuhamasisha timu ya taifa. Alitumia
fursa hiyo kwa kumtungia nyimbo ya kuhamasisha timu yetu ya taifa.
Akiwa na Omari Omari
alimtungia nyimbo nyingi sana ila kwa nyimbo ambazo zilishika soko la mashabiki
ni 'Baada ya kisa mkasa','kifo cha Tx Moshi' pia kamalizi mashairi kwenye wimbo
wa 'kupata majaliwa' baada Omari Omari kulianzi kutunga.
|
MR GOBOLE AKIWA AMEPOZI. |
Aliingiza mijadara
kwa waimbaji mnanda,kila mmoja alimuhitaji kufanya nae kazi,ndipo nae marehemu
Juma Mpogo 'Lupozi' kumuhitaji afanye nae kazi. Ila sasa kwa Lupozi pale
alikuwa anapiga ngoma na visoda,kisha akamtungia nyimbo ya 'mabomu mbagala' na
ile ya 'mabomu gongo la mboto'.
Kwa katika kitongoji
cha Temeke alikubalika na utungaji wake mzuri wa mashairi,pia anawatungia
nyimbo kundi la 'Kombola' lilopo chini ya Hassani Chuna na Masiwa. Kombola nao
aliwatungia nyimbo kama 'subira yavuta kheri' na kisa cha mapenzi.
Anasema kwa kipindi
chote alichokuwa chini ya menejimenti ya marehemu Omari Omari na Juma Mpogo
mziki wa mnanda ulikuwa ni wakipato cha chini hadi kupelekea wakienda kwenye
mashoo huambulia vifedha vya maji ya kunywa na nauli ya kurudi nyumbani.
Hakika gobole amepata
pigo baada ya kufa kwa marafiki wake wapendwa Omari Omari na Juma Mpogo
'Lupozi' na hivi sasa wamempoteza dira kwenye sanaa.
Anasema kama marehemu Lupozi walipiga mkakati
wa kubadiri muelekeo wa kuimba mnanda,ili waimbe taarabu kutokana na yeye
gobole anaweza kutunga taarabu.
Anahisi vifo hivi
vimemrudisha nyuma kutoka hivi sasa anatunga nyimbo na hamna mtu wa wakuimba.
Anaamini wangekuwepo
hai marafiki zake hao,ungekuwa muda mwafaka wa wao kujipatia kipato kutokana na
kipindi kile wao wanaimba mziki huu haukuwa na ela,ila kwa muda huu baada ya
nyimbo zao kuchezwa kwenye kituo cha E.Fm imekuwa sapoti kubwa ya kujitangaza
na kuongeza kipato ukilinganisha na zamani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni