TANGAZA NASI

Breaking

Jumamosi, 14 Novemba 2015

AISHA MTAMU KABISA:- KWA SASA WAKALIWAO MODERN TARADANCE HAPA KAZI TU...SIKILIZA NAJUTA KUPENDA TOKA KWANGU!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


             Muimbaji chipukizi na anaekuja kwa kasi ya ajabu "Aisha mtamu kabisa" tokea wakaliwao modern taradance amesema hiki ni kipindi cha kufanya kazi tu, majungu, kashfa na umimi tupa kule!.

AISHA MTAMU KABISA-MUIMBAJI WA WAKALIWAO.


            Aliyasema hayo wakati alipotembelea ofisi zetu kutambulisha wimbo wake mpya najuta kupenda ambao uliimbwa nae asia utamu hapo kabla, ndugu mwandishi, mimi ni msichana mwenye kipaji na uwezo mkubwa sana na najiamini popote pale kuwa ninaweza na ndio maana hata wimbo huu najuta kupenda nimeufanya tofauti kidogo na ule wa mwanzoni, nawaomba wadau na wapenzi wasikilize kazi yangu na wanipokee kwani mimi sijakuja kubeep katika hii fani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni