TANGAZA NASI

Breaking

Jumamosi, 14 Novemba 2015

WAKALIWAO MODERN TARADANCE KUACHIA NYIMBO MPYA TATU, KATIKA MEDIA MBALIMBALI.LEO.

NA KAIS MUSSA KAIS.


                   Bendi ya wakaliwao modern taradance leo jumapili wanatarajia kuachia nyimbo zao mpya tatu katika media mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi.


THABIT ABDUL-MKURUGENZI WA WAKALIWAO.

         Akizungumza na mtandao huu makini mkurugenzi wa bendi hiyo thabit abdul mkombozi alizitaja nyimbo hizo mpya kuwa ni Najuta kupenda ulioimbwa kwa kurudiwa na Aisha mtamu kabisa, kwangu old fashion iliyoimbwa na kibibi yahya na ukinuna uwe na sababu ulioimbwa nae Aisha othman vuvuzela. aliendelea kwa kusema kuwa tumerekodi nyimbo tano kwahiyo nyimbo zingine mbili ambazo moja imeimbwa na Asia mjusi isemayo kusudi haina pole na mwingine najuta kukufahamu ulioimbwa na hashim saidi igwe tutaziachia hivi karibuni kikubwa ni kuwapa radha tamu na nzuri wapenzi wetu alimaliza kwa kusema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni