Mkurugenzi wa fungakazi modern taarab kapten temba amezungumza na mtandao huu na kusema kuwa wimbo wangu mpya "hata nawe uniseme" ambao ameimba mke wangu zainab machupa ni dongo kwa nyauba flani ambae anapenda sana kunifuatilia.
KAPTEN TEMBA-MKURUGENZI WA FUNGAKAZI MODERN TAARAB |
Aliyasema hayo baada ya kuulizwa swali kwamba mbona maneno yaliyopo katika wimbo huo yanajibu nyimbo mbili za bongo star's modern taarab ambazo ni fisadi kafilisika ulioimbwa na salma sambwanda na funga domo ulioimbwa na salma mikausho?. Akijibu swali hilo temba alisema, unajua ndugu mwandishi siku zote nimekuwa nikionekana mimi temba ni mkorofi lakini ukweli wananichokoza wenyewe! mimi ni mtu muungwana sana tu, sasa huyo nyauba nimempa hiyo hata nawe uniseme kama trellah tu! picha kamili namsubiria anijibu then ataujua moto wangu.
KAPTEN TEMBA. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni