TANGAZA NASI

Breaking

Jumamosi, 21 Novemba 2015

BAADA YA KIMYA CHA MUDA MREFU HATIMAE JUMANNE ULAYA AFUNGUKA NA KUSEMA...........................

NA KAIS MUSSA KAIS.


                  Katika hali ya kushangaza kidogo, yule mpiga gitaa la solo maarufu katika miziki yetu ya taarab nchini Jumanne ulaya ambae yupo ogopa kopa kwa sasa ameupigia simu mtandao huu na kuzungumza yafuatayo.


JUMANNE ULAYA AKIWAJIBIKA STEJI.

                Ndugu mwandishi, mimi Jumanne ulaya sipigi miziki kutafuta sifa hapa nchini isipokuwa nafanya miziki kama kazi yangu niliyoichagua, na pia ni mtu mmoja tu ambae amenipandisha jina langu katika tasnia hii yaani "mzee yusuph" na ndio atakae mudu kunishusha na wala si mwingine. kwanza nilikaa katika bendi yake kwa muda mrefu sana kuliko bendi yoyote ile na pia sitegemei kukaa bendi yoyote kwa muda mrefu tena kama nilivyokaa kwa mzee yusuph. "Narudia tena hakuna wakunishusha mimi J4 na hizo bendi zao za sikukuu na msimu...naomba wapenzi na wadau wangu wasubiri kazi za mikono yangu very soon zitatoka na watajua nina maanisha nini, alipoulizwa ni kwanini anatoa maneno makali kiasi hiki? alijibu neno moja tu kuwa "ipo siku nitaongea".


JUMANNE ULAYA.

              Kuna tetesi za chinichini kwamba Jumanne ulaya haonekani mazoezini ogopa kopa classic na hata katika show za bendi hiyo tena bila sababu kwa uongozi wa bendi, taarifa zisizo rasmi zinasema kuwa kwa sasa yupo mbioni kurudi bendi yake ya zamani Jahazi modern taarab, hebu tusubiri tuone nini atafanya Jumanne ulaya!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni