TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 6 Novemba 2015

HATIMAE YAMETIMIA, MGENI KISODA AITOSA MOYO MODERN TAARAB NA KURUDI JAHAZI RASMI.

NA KAIS MUSSA KAIS.


               Aliekuwa director mkuu wa bendi mpya ya moyo modern taarab mgeni kisoda ameihama bendi hiyo rasmi na kurudi katika bendi yake ya zamani ya jahazi modern taarab inayoongozwa na mfalme mzee yusuph.


         Kisoda alithibitisha hili baada ya kuhojiwa na mwandishi wa habari hizi, na kusema ni kweli kaka mimi kwa sasa ni mwanamuziki wa jahazi modern taarab na nimeanza kazi tokea juzi, nimeamua kuondoka moyo modern taarab ingawa nilikuwa director mkuu pale, na sina matatizo na yeyote kati ya viongozi na wasanii kwa ujumla.haya ni maamuzi yangu tu na nimeyatafakali kwa muda mrefu sana.


     Nawaomba wadau na wapenzi wangu sasa waje huku jahazi modern taarab watanipata kama ilivyokuwa zamani, nawashukuru sana wasanii wenzangu ambao nimewakuta jahazi kwa kunipokea vyema,
kwa upande wangu nawaahidi ushirikiano kama ilivyokuwa zamani, vile vile namshukuru mfalme mzee yusuph na uongozi mzima wa jahazi kwa kunipokea tena.. ikumbukwe kuwa mgeni kisoda kabla ya kuanzisha moyo modern taarab aliwahi kuwa msanii wa jahazi modern taarab lakini alisimamishwa na kufukuzwa kabisa kwa utovu wa nidhamu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni