TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 17 Novemba 2015

BREAKING NEWS:- MASHAUZI CLASSIC KUTOSHIRIKI TAMASHA LA MITIKISIKO YA PWANI 2015.

NA KAIS MUSSA KAIS.


             Bendi ya mashauzi classic modern taradance haitoshiriki tamasha kubwa la mitikisiko ya pwani mwaka huu 2015 linaloandaliwa na kituo cha redio cha times fm cha jijini dar.


WAIMBAJI WA MASHAUZI CLASSIC WAKIWA STEJI.

          Mwandishi wa habari hizi alipata taarifa kutoka kwenye vyanzo vyetu vya habari vilivyopo ndani ya bendi hiyo ndipo zilipoanza taratibu za kutaka kufahamu juu ya jambo hili je lina ukweli wowote?,alipigiwa simu meneja wa bendi hiyo Isumail sumarager na kuulizwa juu ya taarifa hizi, lakini mwanzoni kabisa alionekana kutokuwa tayari kutoa ushirikiano juu ya maswali aliyoulizwa alijibu kuwa yeye hajui chochote na hana taarifa ya jambo hilo lakini baadae alituma sms katika simu ya mwandishi na kuandika meseji hii nainukuu kama ifuatavyo:- "Labda nikufahamishe kwa njia ya meseji ili iwe kumbukumbu nzuri kwako na kwangu ni kwamba tulipigiwa simu kuambiwa kuwa mitikisiko inafanyika tar 12 mwezi wa 12 kwa bahati mbaya tayari tulishapokea pesa ya mtu kwa tarehe hiyo na Isha pia ana kazi ya harusi mombasa tarehe hiyo hiyo na tuliwaeleza times fm kuwa kwa tarehe hiyo tutashindwa kushiriki na walituelewa" mwisho wa kunukuu...sms hii imehifadhiwa katika maktaba ya ofisi yetu kama ilivyo taratibu.


ISHA RAMADHAN MASHAUZI AKIFANYA YAKE STEJINI.

             Kwa maana hiyo mitikisiko ya pwani mwaka huu itashirikisha bendi zifuatazo, Ogopa kopa classic, wakaliwao modern taradance, jahazi modern taarab, excellent modern taarab, Njenje wazee wa kinyaunyau, msagasumu na kibao kata wadau na wapenzi msikose show hii bab-kubwa afrika mashariki na kati siku ya tarehe 12/12/2015 pale viwanja vya dar live mbagala jijini dar.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni