TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 3 Novemba 2015

WAKALIWAO MODERN TARADANCE WAINGIA KATIKA TAMASHA LA MITIKISIKO YA PWANI 2015/2016.

NA KAIS MUSSA KAIS.

             Bendi yako bora na gumzo kwa sasa mjini wakaliwao modern taradance kwa mara ingine tena wameingia katika tamasha bora kabisa afrika mashariki na kati la mitikisiko ya pwani 2015/2016 linaloandaliwa na kituo cha redio cha times fm 100.5 kilichopo jijini dar.

        Akizungumza na mtandao huu mkurugenzi wa bendi hiyo thabit abdul alisema kuwa ubora wa bendi yake na nyimbo zake zinazoendelea kutamba katika media mbalimbali ndio chachu ya mafanikio yao katika kila jambo na pia wadau na wapenzi wetu wamekuwa nasi bega kwa bega katika kutusapoti napenda nichukue nafasi hii kwa niaba ya uongozi na wasanii kuwashukuru sana.

       Alizitaja bendi ambazo zitashiriki tamasha hilo mwaka huu kwa mujibu wa waandaaji kuwa ni Wakaliwao modern taradance, Jahazi modern taarab, Excellent modern taarab, Mashauzi classic na ogopa kopa classic bendi. kiukweli sisi kama wakaliwao tumefarijika sana na tunawaahidi wadau na wapenzi wetu kuwa siku hiyo tutafanya mambo makubwa sana na tutawadhihilishia kuwa sisi ni wa bora kuliko bendi zingine. Tamasha hilo mwaka huu limepangwa kufanyika tarehe 12/12/2015.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni