Bendi ya G5 modern taarab yenye maskani yake mtoni kwa azizi ally jijini dar imepanga mikakati mizito katika kuelekea mwaka mpya 2016.
WAIMBAJI WA G5 MODERN TAARAB.
Akizungumza na mtandao huu makini mkurugenzi wa bendi hiyo Hamisi slim alisema kwa sasa nipo katika kusuka menejimenti yangu ili niweze kufanya kitu kizuri mwakani yaani 2016, unajua ukiwa na timu nzuri yenye viongozi wanaojielewa basi ni rahisi kufanya kitu kizuri, nashukuru kwa sasa nina wasanii wazuri na ambao wanaelewa nini wanatakiwa kufanya, uongozi ndio kitu kilichokuwa kinanipa shida maana mimi nina mambo mengi sana kamwe siwezi kujigawa ni lazima nipate wasaidizi wangu ambao tutakuwa tunapeana majukumu ya kiutendaji na kwa sasa nipo nao tayari kilichopo ni kuanza mikakati mapema.
Bendi ya G5 modern taarab imekuwa ikifanya show zake katika ukumbi wake wa nyumbani yaani ikweta grill mtoni kwa azizi ally kila siku ya jumapili, nenda uwaone mwanahawa chipolopolo, aisha masanja, mwamvita shaibu, ashura machupa, fadhira mnoga na wengineo wakilisongesha gurudumu la G5 modern taarab mbele zaidi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni