TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 7 Desemba 2015

USIKOSE SHOW BAB-KUBWA "USIKU WA MASWAHIBA" WAKALIWAO NA MAPACHA WA TATU NDANI YA MASAI CLUB TAREHE 17/12/2015.

NA KAIS MUSSA KAIS

                 Bendi mbili zinazopiga miondoko tofauti, wakaliwao modern taradance chini yake mkombozi thabit abdul na mapacha watatu inayoongozwa na halidy chokoraa sambamba na jose mara zinatarajia kufanya onyesho la pamoja katika ukumbi wa masai club uliopo kinondoni jijini dar siku ya alhamisi tarehe 17/12/2015.

 

           Wakizungumza kwa nyakati tofauti viongozi wa bendi hizo mbili tukianza na halidy chokoraa yeye alisema nimefurahishwa sana kufanya show hii ya pamoja na bendi ya wakaliwao modern taradance sababu ni miongoni mwa bendi zinazofanya vizuri sana kwa sasa hapa jijini dar hususani katika miondoko ya taarab, unajua thabit abdul ni mpambanaji sana kama nilivyo mimi, namtambua sana tokea tukiwa wote extra bongo na twanga pepeta, nawaomba wapenzi kuja kwa wingi siku hiyo kwani natumaini kutakuwa bab-kubwa.

 

            Nae thabit abdul  kwa upande wake amewaomba wadau na wapenzi wa bendi hizo mbili kutokukosa show hiyo ya kihistoria kwani vijana wake wamepanga kuifunika kabisa mapacha watatu na kuwadhirishia ni kwanini wanaitwa team masauti, wasanii wangu nawaamini sana na hawajawahi kuniangusha hata mara moja hususani linapotokea jambo kama hili la kupiga na bendi ingine.

 

           Show hiyo inayo subiriwa kwa hamu kubwa itafanyika tarehe 17/12/2015 siku ya alhamisi katika ukumbi wa masai club uliopo kinondoni na kiingilio cha mlangoni itakuwa ni shilingi elfu 7000/= tu za kitanzania, wasanii waalikwa siku hiyo watakuwa ni msagasumu na dogo jack simela wa jagwa musica, nyote naombwa kujitokeza kwa wingi sana ili kupata burudani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni