TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 28 Januari 2016

ZAINAB MACHUPA AKANUSHA TAARIFA ZA KUVUNJIKA KWA NDOA YAKE NA KAPTEN TEMBA.

NA KAIS MUSSA KAIS.


                           Muimbaji wa fungakazi modern taarab na mke wa mkurugenzi wa bendi hiyo zainab machupa amekanusha taarifa zilizozagaa kwamba yeye na mumewe kapteni temba ndoa yao imevunjika.

ZAINAB MACHUPA.

                        Akizungumza na mtangazaji wa passion fm warda chande katika kipindi cha ambaa na mwambao siku ya jumatano, zainabu alisema kuwa anashangazwa sana na taarifa hizo zilizozagaa jijini dar kwamba eti amepewa talaka na mumewe kapteni temba baada ya kutokea sintofahamu, akiongea kwa masikitiko zainab alisema kuwa watu wanaitakia mabaya ndoa yao lakini mungu atawalaani na wanalolitaka kamwe halitokuwa.

                 Mtandao huu ulinyanyua simu na kumpigia kapteni temba ili kutaka kujua undani wa jambo hili je kuna ukweli wowote juu ya haya yanayozungumzwa? nae alikuwa na haya ya kusema, mimi na mke wangu zainab tupo katika ndoa bado tunadunda lakini walimwengu wachache wamekuwa wakitufuatilia sana! hivi ikitokea kweli tumeachana kwa mfano wao watafaidika na nini alihoji? mimi sioni mantiki yake! ila huyu ambae anayafanya haya tumeshamjua na mungu atamlaani.

KAPTEN TEMBA.

               Uchunguzi uliofanywa na mtandao huu kupitia watu wa karibu wa familia hii umegundua kwamba temba na zainab hawana maelewano mazuri kwa sasa kitu kilichopelekea zainab kwenda kwa kaka yake kupumzika kwa muda.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni