TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 28 Januari 2016

MDAU ALALAMA KUTAPELIWA LAKI MBILI NA SABINI ELFU NA ACCOUNT FAKE YA MZEE YUSUPH.

NA KAIS MUSSA KAIS.


                   Wizi wa mitandaoni umekuwa ukishamili karibu kila siku na watu wamekuwa wakilizwa sana vitu mbalimbali zikiwemo pesa taslim.


                  Mdau mmoja mkazi wa bagamoyo aitwae mariam "sio jina sahihi" amejikuta akiingia katika mtego huo na kutapeliwa kiasi cha shilingi laki mbili na sabini kupitia account fake ya mzee yusuph mkurugenzi wa jahazi modern taarab ya jijini dar. Akielezea dada huyo alisema kwamba alikuwa akiwasiliana na mtu huyo aliejifanya mzee yusuph kupitia inbox ya account yake ya facebook mpaka kufikia kumpa namba yake ya simu.


             Account hiyo fake imekuwa ikitangaza biashara ya mikoba ya akina mama, viatu pamoja na nguo imekuwa ikionekana katika mtandao wa facebook sana, hivyo mimi nilikubaliana nae aniuzie mikoba ambayo aliniambia ataniuzia shilingi elfu ishirini kila mkoba mmoja kwa bei ya jumla na viatu hivyo nikamtumia pesa hiyo kupitia line yake hiyo ambayo ni "0744-759682" na alikuwa amesajili line hiyo kwa jina la yusuph mohamedy, lakini cha ajabu baada ya kumtumia pesa ile akawa amekata mawasiliano kabisa, ukimpigia simu hapokei anaiacha inaita mpaka inakatika yenyewe ndipo nilipoingiwa na wasiwasi na kuanza kutafuta watu wa taarab ili waweze kunisaidia kumpata mzee yusuph.


            Mtandao huu ulipopata taarifa hizi kutoka kwa huyu dada uliamua kumtafuta mzee yusuph ili aweze kulizungumzia tatizo hili nae alisema, kwanza kabisa hiyo account sio yangu siitambui kabisa, na huyo dada alietapeliwa sio wa kwanza ni wengi sana wamefikwa na tatizo hilo. mimi nilipopata taarifa hizi nilifanya mawasiliano na facebook makao makuu na kuziripoti account zile na kuwaomba wazifungie mara moja kwani zimekuwa zikitumika kwa utapeli, napenda nimpe pole huyo dada pamoja na mwingine yeyote ambae amefikwa na kadhia hii nawaomba wasiamini sana hizi account za watu maarufu humu mitandaoni kwani nyingi zinatengenezwa na wajanja flani ili kuweza kuwaibia au kuwadhurumu pesa au kitu chochote kile alimaliza kwa kusema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni