TANGAZA NASI

Breaking

Jumamosi, 30 Januari 2016

JUMANNE ULAYA "J4" ASIMAMISHWA KAZI NA UONGOZI WA KOLOMBWE MODERN TAARAB!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


                         Mpiga solo mashuhuri nchini tanzania katika tasnia ya muziki wa taarab jumanne ulaya "J4" amesimamishwa kazi kwa kipindi kisichojulikana baada ya kutofautiana na viongozi wake wa kolombwe modern taarab.

               Uchunguzi uliofanywa na dawati la habari la mtandao huu ulibaini taarifa hizi baada ya kufanya upekupeku wake kutoka katika vyanzo vyetu vya habari ambavyo tunaweza kusema kuwa vimetapakaa katika bendi zote za taarab nchini tanzania. Taarifa zinasema kuwa jumanne ulaya amekuwa akilalamika kwanini awekwe katika kolombwe namba mbili na sio namba moja kutokana na hadhi yake aliyonayo katika muziki huu wa taarab nchini, alisikika akilalamika kuwa hii ni dharau kujumuishwa na hawa wasanii wachanga ambao sio hadhi yangu kabisa ni bora hata hii bendi ife tu!.

JUMANNE ULAYA AKIWAJIBIKA STEJINI.
                 Habari hizi zilipomfikia mkurugenzi mkuu Babu chollo ambae yeye anaiongoza kolombwe modern taarab namba moja aliamua kuitisha kikao na viongozi wake wote wa kolombwe zote mbili na kumjadili jumanne ulaya kutokana na kauli zake mbaya ambazo amekuwa akizitoa kila kukicha kwa baadhi ya wasanii jambo linalopelekea morali ya kazi kwa wasanii hao kushuka. maamuzi yaliyofikiwa na uongozi ni kumuondoa jumanne ulaya kabla mambo hayajaharibika.


             Kwahiyo jumapili ya wiki iliyopita wakati wanatoka katika show, kolombwe zote mbili zilikutana na ndipo mkurugenzi mkuu Babu chollo akatumia busara kwa kuwaambia wasanii wa kolombwe modern taarab namba mbili ambayo yupo jumanne ulaya kuwa kuanzia leo naivunja na wasanii wote mkatafute kazi sehemu ingine, lakini lengo lilikuwa ni kumuondoa J4 kibusara ili wasanii wenzake wasione kuwa kadharauliwa.

             Jumanne ulaya alipofika nyumbani kwake na kutafakali kwa kina kauli ya mkurugenzi Babu chollo aliamua kumtumia sms mkurugenzi huyo ambayo ilikuwa ikisomeka kama ifuatavyo nanukuu:-

          "Mtu wangu maamuzi yako yapo sahihi, tupo pamoja ila kukaa isiwe kigezo bendi zote za taarab nilishawahi kufanya hivyo, melody, jahazi na zingine zingine nyingi kwenye taarab. isitoshe hata mziki ulikuwa unapigwa unakatisha tamaa na nilikuwa hapa kwa kukuheshimu tu nna njaa nna dhiki sana sio kwa bendi na mziki huo maadamu tupo hai tutaonana ila imenifurahisha sana ili niondokane na kujichoresha na miziki ya akina yahaya".



BABU CHOLLO-MKURUGENZI WA KOLOMBWE MODERN TAARAB.
                  Dawati la mtandao huu lilifanya mahojiano na mkurugenzi mkuu wa kolombwe modern taarab Babu chollo kuhusu habari hii ambae alisema kuwa amemuondoa kabisa katika bendi yake jumanne ulaya kwa utovu wake wa nidhamu. Nimemvumilia sana jumanne ulaya lakini sasa imefikia mwisho ni vyema aende huko anapoona kuna hadhi yake na aniachie bendi yangu, mbona mimi nimekuwa nikimsaidia bila kujali nini wala nini, alikuja kwangu akasema kuwa kodi ya nyumba imeisha anataka laki tatu, mimi nikampa laki mbili na nusu nikamwambia jumapili ya wiki iliyopita nitammalizia hamsini iliyobaki na hii yote nafanya kutokana na umuhimu wake katika bendi, nimekuwa nikimlipa elfu ishirini kila show kuanzia jumanne mpaka jumapili ambazo ni sawa sawa na laki moja na ishiri kwa wiki moja tu!...haya nimjali vipi tena mtu kama huyo?, aende tu mimi sina mjadala na yeye, aende hata huko jahazi modern taarab ambapo amekuwa haishi kukutaja kila wakati alimaliza kwa kusema.

                 Alipotafutwa jumanne ulaya ili ajibu haya aliyoyasema mkurugenzi babu chollo, yeye alianza kwa kusema kuwa hakuwa ameajiliwa pale kolombwe sasa wanawezaje kunisimamisha au kunifukuza bendi? alihoji, ile ni bendi ya ndondo tu ambayo msanii yeyote anaweza kwenda kupiga. unajua ndugu mwandishi nikwambie jambo moja bendi ile haina nidhamu kabisa, wasanii wake wanagombana steji kila wakati, walevi wana uwezo mdogo sana kulinganisha na mimi...siwezi kuendelea kujidhalilisha kwa kupiga katika bendi kama ile. kuna huyu jamaa anaitwa yunus sijui ndio nani...mimi simtambui anasema kuwa amenisimamisha bendi, yeye ni nani katika bendi? alihoji maana simtambui. waache waendelee ila mimi nakataa hawajanifukuza wala kunisimamisha kwani sina mkataba nao kabisa mimi alimalizia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni