TANGAZA NASI

Breaking

Jumamosi, 30 Januari 2016

ALLY J AKANUSHA UVUMI ULIOZAGAA JIJINI KUWA ANAELEKEA DAR MODERN TAARAB.

NA KAIS MUSSA KAIS.


                 Mpiga kinanda maarufu na mkurugenzi wa five star's modern taarab ally j leo kupitia mtandao huu amekanusha uvumi uliozagaa jijini kuwa yupo katika mazungumzo ya kujiunga na bendi ya dar modern taarab iliyo chini ya mkurugenzi Alhaji Abdallah feresh.

ALLY J-MKURUGENZI WA FIVE STAR'S MODERN TAARAB.
               Akionyesha kushangazwa na habari hizi ally j alisema si kweli huo ni uvumi tu ambao hauna ukweli wowote ule, mimi pale dar modern huwa nakwenda nina marafiki zangu na walimu wangu akina mlamali adam sasa kuna ajabu gani kwa mimi kwenda pale? alihoji, na kama kweli itakuwa hivyo kwa bendi yoyote ile hata kama isiwe dar modern mimi sina tatizo kikubwa tukubaliane kimasharti katika utendaji wa kazi.

          Maana mimi kama ally j nina wasanii na watu kadhaa ambao wananiangalia mimi kwahiyo nitakapokwenda kokote pale lazima niwe nao hivyo ni lazima sio hiari, baada ya hapo mambo mengine yatafuata. Abdallah feresh ni mzee wangu na tunaheshimiana ila hajawahi kunitamkia kuwa ananihitaji katika bendi yake hizo ni tetesi ambazo mimi nazikanusha leo. Aliendelea kwa kusema kuwa kwa sasa amejikita katika biashara zake zaidi na muziki ameuweka pembeni kwa muda ila inapotokea issue basi anafanya kwa kuwa muziki upo damuni zaidi.

            Alichukuwa nafasi hiyo kuwaasa wasanii wa muziki huu wa taarab kuacha kubweteka na badala yake wajikite sana katika kufanya biashara kwani mwisho wa siku msanii anapozeeka anakuwa ni mfano mbaya kwa kile alichochuma katika muziki, mifano mingi tunaiona kwa wazee wetu waliotutangulia katika muziki hapa nchini alimalizia kusema Ally J.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni