TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 2 Februari 2016

HAMISI SLIM:- HII NDIO SABABU KUBWA INAYOPELEKEA BENDI NYINGI ZA TAARAB NCHINI HAZIFIKI MBALI.

NA KAIS MUSSA KAIS.


HAMIS SLIM-MKURUGENZI WA G5 MODERN TAARAB

                  Mkurugenzi wa bendi ya G5 modern taarab Hamisi slim au ukipenda unaweza kumuita "mzee wa manyamnyam" amezungumzia sababu zinazofanya bendi nyingi za taarab nchini hazifiki mbali katika safari ya mafanikio.


                  Akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika maeneo yake ya kujidai ikweta grill mkurugenzi huyo kwanza kabisa aliainisha sababu tatu kuu zinazofanya bendi nyingi zisiendelee kama yalivyo malengo yao waliyojiwekea. 1.Wakurugenzi karibia wote wanapoanzisha bendi zao huwa wanafikilia kuchukuwa wasanii kutoka katika bendi zilizofanya vizuri japo kidogo kwa kisingizio kwamba nazo zitajikongoja kwa uzoefu wa wasanii hao matokeo yake wasanii wanaingia katika bendi kwa tamaa ya pesa na wala hawajitumi na hawajali kuwa wewe umepoteza kiasi gani katika kuisuka bendi hiyo. 2. Kambi inayowekwa na uongozi kwa ajili ya wasanii hao huwa inatumia kiasi kikubwa sana cha pesa hali inayopelekea kutengwa bajeti kubwa sana na mategemeo ya uongozi na mkurugenzi ni kuwa watapata pesa hizo katika uzinduzi, baadhi ya gharama zinazotumika katika kambi ni maradhi kwa wasanii, vyakula, kurekodi audio pamoja na video albam nzima na gharama nyinginezo nyingi. 3. Uzinduzi...hapa ndipo kwenye mtihani mkubwa ambapo bendi inaweza kufeli au kufaulu kulingana na uzinduzi utakavyopokelewa na mashabiki, ukifanya vibaya ndio shimo au kaburi la bendi yako na ukifanikiwa kufanya vizuri ndipo unapoweza kupanga mikakati ya nini cha kufanya baada ya hapo.


           Lakini kilichopo bendi karibia zote huwa zikifika katika hatua hiyo ndipo habari yao inapokuwa imeishia kinachobakia ni ubabaishaji tu wakubahatisha ni wapi nitafanikisha kupata wapenzi wakuweza kuingia katika show yangu. Kikubwa kinachokwamisha ni pesa za maandalizi ya show, viongozi wengi wa mabendi wanapofikia hapo akili zao zinashindwa kufanya mchanganuo wa haraka kuweza kubaini kwamba hapa tunatakiwa tuwe na show zetu wenyewe kwa muda japo miezi mitatu bila kusimama ili wadau na mashabiki waendelee kutupa sapoti zao!, utakuta kiongozi anakwambia tayari tumeshazindua kwahiyo kilichobakia ni kusubiri mapromota waje kununua show katika bendi...hili ni tatizo ambalo lipo katika bendi zote za taarab nchini, bendi nyingi zitaendelea kufa na kupotea kabisa katika ulimwengu huu wa muziki wa taarab nchini sababu viongozi wake na wakurugenzi hawapo makini katika utendaji wao, wataendelea kufanya kazi kwa hasara sababu hawajitambui.


            Kikubwa tunatakiwa tuamke sasa kama kweli tunataka tufike mbali na kuzipatia maendeleo bendi zetu, hatujachelewa bado wakati ndio huu...Tusipo uanika tutautwangwa mbichi alimaliza kwa kusema mkurugenzi huyo!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni