TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 2 Februari 2016

KONGAMOYO BENDI NA SABAHA MUCHACHO KUITIKISA LANGO LA JIJI MAGOMENI KWA BURUDANI LEO JUMATANO NA KILA JUMATANO.



NA KAIS MUSSA KIS.

               Bendi ya kongamoyo music yenye maskani yake magomeni jijini dar inaanza rasmi kutumbuiza katika ukumbi wa lango la jiji magomeni mikumi siku ya leo jumatano tarehe 3/2/2016.

             Akizungumza na mtandao huu mkurugenzi wa bendi hiyo mr Iqbar alisema kuwa wamepania kwa kiasi kikubwa kuwathibitishia wadau na wapenzi wa taarab hizi za zamani yaani "old is gold" kuwa wao kongamoyo ni mabingwa kwa kipindi hiki wa kupiga taarab hiyo na wala si vinginevyo. unajua watu wamezoe kuona bendi moja au mbili hapa jijini dar zikisifika kwa kupiga taarab hizi za zamani lakini nakuthibitishia ndugu mwandishi kwamba siku ya leo wadau watajua ubora wetu na kwanini kongamoyo tumekuwa tukipata mialiko mbalimbali ndani ya nchi na nje ya nchi.

THANIA MSOMALI NA MWASITI SULEIMAN WAIMBAJI WA KONGAMOYO.

            Msanii mwalikwa atakuwa ni mama yetu sabah salum muchacho ambe ataimba nyimbo zake zote kali na ambazo zimekuwa zikitamba katika vituo mbalimbali vya redio na kumbi za burudani, kikubwa nawaomba wapenzi wajitokeze kwa wingi ili waje kupata burudani nzuri ambayo walikuwa wakiikosa kwa muda mrefu sana, sisi kongamoyo tutakuwa tunapiga lango la jiji magomeni kila jumatano kuanzia tarehe 3/2/2016 hii na ikumbukwe kuwa hii ni program endelevu alimaliza kwa kusema.

SHINUNA KASSIM NA ASYA UTAMU WAIMBAJI WA KONGAMOYO.

             Katika show hiyo kiingilio kitakuwa ni shilingi elfu 5 mlangoni kwa mtu mmoja. Kabla ya kongamoyo kuanza kutumbuiza katika ukumbi huo, bendi ya Aljazeera walikuwa wakitumbuiza hapo kwa siku hii hii ya jumatano lakini kilichowaondoa inakuwa bado ni kitendawili, wewe na mimi hatujui ila mtandao huu utafuatilia alafu utakuja kuwajuza wasomaji wake hapa hapa ni nini kimewakuta.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni