TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 21 Februari 2016

HAPPY BIRTHDAY MKURUGENZI WA MTANDAO WA UBUYU WA TAARAB KAIS MUSSA KAIS "SKILLMAN".

NA DAWATI LA HABARI.


                 Leo tarehe 22/2...ni siku nzuri na muhimu sana kwa mkurugenzi wetu wa mtandao huu wa ubuyu wa taarab kais mussa kais "skillman" kwani anasherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kuweza kutimiza umri wa miaka kadhaa.


              Chumba cha habari cha mtandao huu tunapenda kuungana na mkurugenzi wetu kais mussa kais katika kusherehekea kwa pamoja.Akiizungumzia siku hii kais alisema kuwa imekuwa ni 50/50! furaha kiasi lakini kwa upande mwingine ni huzuni kwani pamoja na kuzaliwa siku hii lakini pia nilioa siku kama ya leo marehemu mke wangu nyawana isale!, na jambo la kustaajabisha ndoa ile ilikuwa ifungwe tarehe za nyuma lakini nyawana aliniomba tusubiri siku yangu ya kuzaliwa ndio tuoane ili ziwe sherehe mbili kwa pamoja na kweli ndivyo ilivyokuwa!, mwenyezimungu namuomba amsamehe madhambi yake na ampe kivuli miongoni mwa vivuli vya peponi...Amin!.


              Katika kusherehekea siku hii ya kuzaliwa kwa mkurugenzi wetu kais mussa kais "skillman" sisi kama wafanyakazi wake tumemuandalia party ya nguvu katika ufukwe wa bamba beach kigamboni ambapo burudani mbalimbali zitakuwepo. Happy birthday mkurugenzi kais mussa kais "skillman".

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni