TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 23 Februari 2016

MGENI KISODA:- MOYO MODERN TAARAB HAIWEZI KUENDELEA, SABABU WANAFIKI WAMEMZUNGUKA SAIDI FELLAH!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

               Aliekuwa director wa bendi ya moyo modern taarab lakini kwa sasa yupo jahazi modern taarab Mgeni kisoda leo hii amevunja ukimya na kutoa la rohoni kuhusu bendi yake hiyo ya zamani.

MGENI KISODA AKIWA TAYARI KWA KUPANDA NDEGE.

            Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mgeni kisoda alisema, unajua mimi ndio nilimfuata saidi fellah na kumshauri ni vyema tukaanzisha bendi ya taarab ndani ya kambi ya mkubwa na wanawe nae alinielewa na kweli bendi ikaanza chini ya uongozi wangu. nilijitahidi kutafuta wapiga vyombo na baadhi ya waimbaji wazoefu ndipo kambi rasmi ikaanza kutengeneza nyimbo mpya za bendi.

               Wakati tupo kambini maneno ya chini chini yakaanza kuzungumzwa na wasiopenda maendeleo, eti kwa nini ndani ya mkubwa na wanawe kuwe na mameneja zaidi ya mmoja, au kuwe na viongozi wengine upande wa taarab wakati hii ni familia moja!, wanashindwa kuelewa kuwa kuongoza bongo fleva sio sawa na kuongoza taarab! muziki wa taarab unatakiwa fitina ya hali ya juu zaidi kusimamisha bendi!. Hata pale tulipokwenda kufanya utambulisho wa bendi pale dar live kuna baadhi ya viongozi wa yamoto hawakupenda kabisa sisi kufanya show jukwaa moja na yamoto!.

MGENI KISODA AKIWA NDANI YA NDEGE.

             Mimi nilipoona matatizo yanazidi ndipo nilipoamua kuondoka na kuwaacha waendelee lakini matokeo yake mpaka sasa hakuna kinachoendelea pale, nyimbo tulizotengeneza mpaka sasa hazijarekodiwa, sidhani hata kama mazoezi wanafanya, mkurugenzi alijitahidi kila tulichokuwa tunamuambia atununulie alikuwa akinunua kwa ajili ya moyo bendi, mimi nawaambia waendeleze pale nilipoacha mimi kama kweli wanaweza! waache maneno ya kinafiki na wivu usio na maendeleo, taarab sio sawa na bongo fleva alimaliza kwa kusema Mgeni kisoda!.

           

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni