TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 24 Februari 2016

KUFUATIA MATUSI YANAYOENDELEA MITANDAONI, MZEE YUSUPH AZUNGUMZA NA UBUYU WA TAARAB NA KUSEMA.....

NA KAIS MUSSA KAIS.


                 Takribani wiki nzima sasa mtandao wa instagram umekuwa ndio habari ya mjini kutokana na matusi, kashfa na kubebeduana kunakoendelea baina ya mke wa mzee yusuph leyla rashid na dada wa mfalme ambae ni muimbaji aitwae khadija yusuph.

MZEE YUSUPH, KHADIJA YUSUPH PAMOJA NA MKEWE LEYLA RASHID.


               Team za wawili hao zimekuwa zikitandaza kejeli na matusi kwa kila kundi kumtetea yule wanae mshabikia, khali iliyopelekea khadija yusuph nae kujibu kutokana na kuzidiwa hasira kwa matusi yanayoendelea dhidi yake!, mtandao huu kama kawaida yake ulimtafuta mzee yusuph kwa simu na alipopokea alisema yupo arusha na amekwenda kwa shughuli zake, ndipo swali la msingi lilipo ulizwa na mwandishi je yeye kama mume na kaka wa familia anaizungumziaje khali hii inayoendelea mitandaoni hususani kwa dada yake na mkewe kudhalilishana na kunyambuana kusipo na faida kwa jamii mpaka kufikia kuguswa na wazazi kwa matusi hayo?.


LEYLA RASHID MKE WA MZEE YUSUPH.

          Kwanza kabisa mfalme alianza kwa kusema kwamba anahudhunishwa sana na hali hiyo na katika maamuzi wala hatoegemea upande wowote sababu wote ni wakosa, familia yangu imekuwa mfano wa mtu alievuliwa nguo!, matusi mazito yamekuwa yakitukanwa mpaka mama yangu ameingizwa humo maskini ya mungu!, mimi nimeshazungumza na kila mmoja kwa wakati wake na nimewaambia sitaki kuona tena hali ile ikijirudia!, pia nachukuwa nafasi hii kuziasa zile team za kila mmoja kati yao kuacha mara moja kutukana au kumkashifu mmoja wapo kati yao! siku zote wasanii wanatakiwa kuwa kioo cha jamii sasa inapokuwa tofauti kwakweli inakuwa haipendezi.


KHADIJA YUSUPH DADA WA MZEE YUSUPH.

          Nawaomba wadau na wapenzi wa jahazi modern taarab, wapenzi wa mke wangu Leyla rashid, wapenzi wa dada yangu khadija yusuph wote kwa pamoja tusahau tofauti zetu na tupendane na kuacha huyu pepo mmbaya apite kabisa maana kwa sasa hali si shwari, nimehudhunishwa na matusi yanayoshushwa dhidi yangu lakini yote namuachia mungu kwani yeye ndio mhukumu wa kila jambo alimaliza kwa kusema mfalme mzee yusuph.


        Mtandao huu utaendelea kuwatafuta leyla rashid na hadija yusuph ili nao kwa pamoja watoe dukuduku zao za rohoni na waswafiane nia kwani wao ni ndugu kwa sasa! wameunganisha undugu kupitia mzee yusuph pamoja na watoto ambao amewazaa bibie leyla rashid.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni