TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 4 Februari 2016

HATIMAE KAPTEN TEMBA AKILI KUMUACHA ZAINAB MACHUPA KWA TALAKA MOJA!, SABABU KUBWA NI......!!

NA KAIS MUSSA KAIS.


                  Kile kizungumkuti kilichokuwa kikiwasumbua wadau juu ya tetesi zilizozagaa juu ya kuvunjika kwa ndoa ya mastaa kapten temba na zainab machupa toka fungakazi modern taarab, leo kimepata jibu kamili.

KAPTEN TEMBA AKIWA KATIKA POZI LA NGUVU.


                Akizungumza na mtandao huu kapten temba alisema kuwa amemuacha zainab machupa tokea tarehe 7/1/2016 na kumrudisha nyumbani kwa wazee wake kwa wema kabisa, alipoulizwa na mwandishi wa habari hizi ni nini sababu iliyopelekea wakaachana? alijibu hawezi kuanika sababu hizo mitandaoni au kwa waandishi wa habari isipokuwa ijulikane kuwa zainab aliiomba talaka nami nikampatia baada ya suluhu kukosekana.


            Jambo lingine ni kwamba hii ni hali ya kawaida wala sisi sio wa kwanza kuachana kwahiyo wadau nawaomba wasiichukulie hali hii kama ni issue kubwa sana wajue tu ridhiki imeisha kati yangu na zainab ndio maana tumeachana. Kwa upande wa zainab yeye alisema tu kuwa alichozungumza kapten temba ni sahihi kwahiyo hana cha kuongeza hapo.


ZAINAB MACHUPA MTALAKA WA KAPTEN TEMBA.

             Wakati huo huo kuna taarifa zinadai kwamba kapten temba amekuwa akimtuhumu senior bachelor kwamba amekuwa akisambaza habari za temba kuachana na zainab kwa wandishi wa habari na kupelekea senior na temba kutumiana sms za matusi na kashfa nzito ambazo kimaadili haziwezi kuwekwa hapa mtandaoni, alipoulizwa temba alisema kuwa hayupo tayari kuzungumza lolote juu ya mtu huyo yaani senior bachelor. Baadae alitafutwa senior kwa simu yake ya mkononi lakini ilikuwa ikiita tu pasipo majibu yoyote, tunawaahidi kumtafuta senior bachelor ili azungumzie taarifa hizi zilizozagaa jijini kwa sasa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni