TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 10 Februari 2016

MKURUGENZI WA MAJAZ MODERN TAARAB HAMISI MAJALIWA AKANA TAARIFA ZA MPASUKO NDANI YA BENDI YAKE!.

NA KAIS MUSSA KAIS.



                            Taarifa zilizozagaa miongoni mwa wadau wa taarab nchini tanzania kuwa bendi ya majaz modern taarab ina mpasuko mkubwa wa pande mbili yaani upande mmoja kuna wasanii ambao wana mkubali sana Ashura machupa na upande wa pili wapo wanaomkubali sana senior bachelor, leo umekanushwa na mkurugenzi wa bendi hiyo Hamisi majaliwa.

WAIMBAJI WA MAJAZ MODERN TAARAB.

                   Akizungumza na mtandao huu mkurugenzi huyo alisema kuwa ameshangazwa sana na taarifa hizo kwani mpaka juzi tu alikuwa nao viongozi hao nyumbani kwake wakipanga mikakati ya kuifikisha mbali zaidi bendi hiyo, hizo taarifa sio za kweli kabisa mimi kama mkurugenzi wa bendi hii nakanusha hakuna kitu kama hicho katika bendi yangu alisema.

ASHURA MACHUPA-MKURUGENZI MSAIDIZI WA MAJAZ

            Tukirudi nyuma kidogo mtandao huu ulipata taarifa kuwa bendi ya majaz modern taarab wakati ipo ziarani mafia kikazi kulitokea sintofahamu baina ya viongozi wawili hao yaani Ashura machupa na Senior bachelor juu ya mapato ya mlangoni yaliyopatikana katika show ya kwanza kabisa, inasemekana "team senior bachelor" Abdallah kitawine na Ochu kilimba ndio waliokaa mlangoni kupokea kiingilio lakini mwisho wa show pesa iliyoonyeshwa na watu hao haikulingana na idadi ya watu walioingia, tatizo ndipo lilipoanzia mpaka kurushiana maneno.

          Katika show ya pili ikaonekana ni vyema sasa awekwe mtu wa Ashura machupa mlangoni ili kupokea kiingilio ili waone tofauti yake!. mtandao huu ulipopata taarifa hizi ulimuendea hewani mtu aitwae "Afsa moge yakusela" ambae inasemekana ni msemaji wa Ashura machupa na meneja wake ilikuzungumzia hili linalomuhusu msanii wake, Moge alianza kwa kusema kuwa taarifa hizo ni kweli na baada ya kuona wametupiga yaani wametudhurumu mapato ya mlangoni katika show ya kwanza waliamua kuniweka mimi mlangoni!, hawa jamaa sio wazoefu katika kazi hii kama nilivyo mimi na ndio maana wamesababisha mpasuko mkubwa baina ya viongozi hawa wawili.

SENIOR BACHELOR- DIRECTOR WA MAJAZ MODERN TAARAB

          Alipopigiwa simu Senior bachelor yeye alisema kwamba hakuna mpasuko na wala hakutotokea mpasuko wowote katika bendi na hayo anayoyasema huyo afsa moge sio kweli kabisa!, mtandao huu ulimuuliza juu ya taarifa za yeye senior kugombana na afsa moge mpaka kufikia kurushiana maneno makali, alikili kuwa ni kweli hilo lilitokea ila ni kawaida kunapokuwa na watu wa tabia tofauti ila kwa sasa yamekwisha.

           Mtandao huu uliamua kumrudia tena mkurugenzi hamisi majaliwa na kumuuliza huyu afsa moge yeye ni kama nani katika bendi yake? nae alikuwa na haya ya kujibu:- huyo jamaa hana cheo chochote katika bendi hii, nijuavyo mimi ni rafiki wa Ashura machupa tu, sijui ni meneja wake sijui nini mimi sijui! hana uwezo wa kuizungumzia majaz modern taarab kwa njia yoyote ile maana simtambui katika uongozi wangu, meneja mkuu wa bendi hii ni Abdallah kitawine na meneja msaidizi ni Ochu kilimba basi naomba ieleweke hivyo!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni