TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 10 Februari 2016

MJUE FARIDA AU MAMAA MUSHKERI AKIWA NA KAHAMA MODERN TAARAB TOKA MKOANI SHINYANGA!.


NA KAIS MUSSA KAIS.

MASHABIKI WAKISEREBUKA.

                  Muziki wa taarab kwa sasa umeweza kupanua wigo mpana sana na kusambaa karibia tanzania nzima na jambo la kujivunia zaidi ni pale ilipoanzishwa bendi ya kwanza ya taarab kahama mkoni shinyanga iitwayo kahama modern taarab.

            Farida mamaa mushkeri ni mwanamke wa kwanza kabisa kuthubutu na kufungua bendi yake mwenyewe ya taarab iitwayo kahama modern taarab yenye wasanii 12 mpaka sasa na imeanzishwa mwaka 2015 yaani ina mwaka mmoja tokea imeanzishwa. lakini kabla ya kuanzisha bendi yake mwenyewe Farida amepitia bendi ya kagera modern taarab na mwanza modern taarab.

FARIDA "MAMAA MUSHKERI" MKURUGENZI WA KAHAMA MODERN TAARAB.

           Mpaka sasa bendi hii imesharekodi nyimbo 2 ambazo zote zimeimbwa nae Farida ambazo ni "hasidi hana hila" na "ufitini hauna tiba" zilizorekodiwa huko huko kahama mkoani shinyanga.kwa sasa bendi hii ipo kambini kuandaa nyimbo zingine nne ili kukamilisha albam yenye nyimbo 6, Farida anaendelea kwa kusema kuwa anaomba wafadhili wajitokeze ili kumpa sapoti kwani amekuwa akiingoza bendi hiyo katika mazingira magumu sana sababu hana msaada toka kokote pale.

           Angefurahi zaidi kama ataweza kupata mfadhili ambae watakaa chini na kupanga kwa pamoja nini cha kufanya ili kuweza kuipeleka mbele zaidi kahama modern taarab, yeyote ambae atahitaji kuwasiliana na Farida "mamaa mushkeri" basi anaweza kumpigia simu kwa namba hizi zifuatazo:- 0713-332813 au 0755-360113, katika ndoto zake anasema atafurahi sana kama atatengenezewa japo wimbo mmoja na thabit abdul mkombozi. Huyo ndio Farida "mamaa mushkeri" mkurugenzi na muimbaji wa kahama modern taarab yenye maskani yake mkoani shinyanga tanzania.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni